MIMBA YA JINI -12

Author

Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini -12-

SASA SIKIA ILI USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA #LIKE PAGE HIII MWENDELEZO WA HADITHI HII YOTE USIKUPITE sorry kwa kurudia kipande cha 11 mwendelezo huu hapa SHARE ZIKIFIKA 250 NAPOST KIPANDE CHA 13 NASUBIRIA SHARE ZIFIKE 250 NIPOST

ILIPOISHIA:

Aliushangaa uwezo wa Shehna wa kuelewa vitu vingi vinavyoonekana na vilivyojificha. Alikuwa

amefanya siri ambayo hata mkewe na watu wengi hawakuijua kama ana nyumba ndogo. Lakini

yeye aliijua bila kumwambia, alijiuliza ni nani kwenye uganga hayupo kwa vile alionekana

mwanamke mrembo tena mwenye kujipenda.

SASA ENDELEA...

Tofauti na waganga wengi ambao wengi wao huwa hawajipendi, mavazi yao huwa ya kujiachia wala hawajui mapambo na manukato.
"Sasa Shehna ni nani...au jini? Ha...hapana huko nimefika mbali," Mustafa alijiuliza na kukataa mwenyewe.
"Mbona jana niliota nimelala naye sehemu nzuri lakini nilipoamka nilijikuta nipo nyumbani kwangu? Na Shehna alirudi saa ngapi na kwa nini hakuniamsha mpaka niliposhtuka asubuhi na kujikuta nimetumika kutokana na kufanya naye mapenzi ya ndotoni.
"Mmh! Shehna mbona anataka kunipa mtihani mzito, anataka nizae naye kwa ahadi ya kumpatia mtoto kupitia kwa mke wangu. Sasa mbona ametaka azae yeye kwanza? Mmh! Kazi ipo."
Alijikuta amefika hospitali bila kupata jibu kitu kinachomtatiza kuhusu Shehna. Aliingia hospitali na kwenda chumba alicholala mkewe, alimkuta akiwa amejiandaa kutoka baada ya kupewa ruhusa mapema.
"Yaani mume wangu unajua naumwa unaniacha mpaka saa hizi?" Husna alimuuliza kwa hasira.
"Tabia hii imeanza lini, hata salamu unafikia kunilaumu, ningekufa ungefurahi?" Mustafa alijibu kwa hasira.
"Ufe na nini?"
"Kwa vile hukutaka kujua haina muhimu, unaendeleaje?" Mustafa naye alikuwa mkali kwa mkewe.
"Nisamehe mume wangu nilichanganyikiwa baada ya kuchelewa kukuona wivu uliniingia, ulipatwa na nini mume wangu?"
"Ilitakiwa tusalimiane tujuliane hali kisha tuzungumze mambo mengine."
"Ni kweli, nisamehe mume wangu nimekosa wivu wakati mwingine ugonjwa."
"Nimekukataza mara ngapi sipendi wivu wa kijinga, kila siku umekuwa ukiniona akili yangu unawaza ujinga."
Mustafa alimjia juu mkewe kwa vile alikuwa amepata nafasi, naye alikuwa amechoka na wivu wa kijinga wa mkewe ambao uligeuka kero kitu kilichosababisha kuanzisha uhusiano na mwanamke ambaye mkewe alimshtumu anatembea naye. Mwanamke huyo ilitokana na kushtumiwa na mkewe kwa hisia bila ukweli.
Kwa hasira alifanya kweli kwa kutembea na yule mwanamke ambaye baadaye alimfanya nyumba ndogo na kumuhamisha mtaa ule na kwenda kumpangia sehemu nyingine na kuendeleza mapenzi kwa siri.
Siri ile aliijua peke yake hata rafiki yake hakujua kama ana nyumba ndogo, lakini alishangaa Shehna kuijua.
"Mume wangu huna dogo, nimekosa nisamehe."
"Sawa, vipi unaendeleaje?"
"Namshukuru Mungu sijambo japokuwa mwili hauna nguvu."
"Pole mke wangu, wakati nakuja kuna mwendesha pikipiki alijigonga kwenye gari langu, watu wakajua nimemgonga wakataka kunipiga lakini askari wa barabarani alifika na kuniokoa," Mustafa alitengeneza uongo ili kumpoza mkewe.
"Jamani pole mume wangu!" Husna alisema kwa sauti ya huruma.
"Asante."
Mustafa alimchukua mkewe na kurudi naye nyumbani, alipofika alijikuta akitaka kujua kipi kilimfanya akaidi amri ya Shehna. Baada ya kutulia kwa muda alimsemesha mkewe.
"Mke wangu."
"Abee, mume wangu."
"Kipi kilichokufanya umuue mtoto wangu?"
"Mume wangu kupima ujauzito ni kumuua mtoto?" Husna alishtuka.
"Shehna alituambia nini?"
"Mume wangu utaamini vipi una ujauzito bila kupima?" Husna alijitetea.
"Si alitukataza?"
"Ndiyo! Lakini bado nilishindwa kumuamini, mume wangu kwanza Shehna ni nani mbona masharti yake ya ajabuajabu?"
"Mke wangu tumehangaika sehemu ngapi tumepewa masharti mangapi tuliyoyatekeleza, yaani hili ndilo umeliona gumu?"
"Mi nimechoka kila siku masharti magumu."
"Ha! Mke wangu umeweza kulala makaburini kutafuta mtoto, umeona kazi kutotumia dawa za kizungu ikiwa hali yako ilikuwa nzuri?"

Itaendelea NASUBIRIA SHARE ZIFIKE 250 NIPOST MWENDELEZO WAKE #LIKE PAGE USIPITW NA KIPANDE HATA KIMOJA

0 comments:

Post a Comment