Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini -11
Mtunzi: #Mzizi_Mkavu
SASA FANYA HIVI ILI USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA #LIKE_PAGE HII KISHA SHARE HADITHI HII NASUBIRIA #SHARE 250 NIPOST NYINGNE ONYESHA UPENDO TWENDE SAWA
ILIPOISHIA:
"Mustafa mimi mtu wa kawaida najua uzuri wangu utakubabaisha, nione kama nyama yoyote isiyo na mfupa kwenye kisu kikali."
"Unatu..tumia kinywaji gani?" Mustafa alijikaza na kumuuliza.
"Kwa leo sihitaji chochote nataka tuzungumze kitu ili niondoke zangu."
"Kitu gani?"
"Mustafa unakumbuka nilikuahidi nini?"
SASA ENDELEA...
"Vingi, sijui kipi kimoja wapo."
"Kuhusu matatizo yako."
"La kunipatia mtoto."
"Umempata?"
"Sijampata."
"Kwa nini?"
"Hatukufuata ushauri wako."
"Toka muanze kuhangaika mkeo aliwahi kupata dalili za ujauzito?"
"Hapana."
"Kwa hiyo kazi yangu nilimaliza?"
"Bado kwa vile sijapata mtoto."
"Utapata vipi na mkeo hataki mtoto?"
"Sasa utanisaidiaje?"
"Mustafa naomba sasa hivi unisaidie nilichokuomba."
"Kama kitu kimo ndani ya uwezo wangu nitakusaidia."
"Nataka mtoto," Shehna alisema huku akimtazama kwa macho yake ya huruma yaliyojaa mahaba.
"Mtoto!" Mustafa alishtuka.
"Ndiyo."
"Mimi nitampata wapi?"
"Unawezaje kumpatia mkeo mtoto?"
"Kwa kukutana kimwili."
"Basi na mimi namuhitaji kwa njia hiyo."
"Yaani mimi nifanye mapenzi na wewe?"
"Ndiyo, kwani kuna ubaya?"
"Si unajua mimi ni mume wa mtu?"
"Mustafa hujawahi kutembea nje ya ndoa yako?"
Swali lile lilimfanya apate kigugumizi kulijibu kwa vile alikuwa na mwanamke aliyempangia chumba na siku nyingine alikwenda kulala kule na kudanganya amekwenda safari ya kikazi.
"Mustafa unaiheshimu sana pete ya ndoa kwa vile mkeo ni mkorofi na ana wivu sana, lakini huiheshimu ndoa yako. Au mimi kutaka kuzaa na wewe umeniona malaya?"
"Ha...ha...pana Shehna sijakufikiria hivyo."
"Sasa nipe jibu moja, utanipatia mtoto au hunipi?"
"Nitakupatia."
"Nimefurahi kusikia hivyo, nakuahidi kukupa zawadi kubwa sana katika maisha yako."
"Nitafurahi sana."
"Mustafa natoka mara moja nitarudi muda si mrefu."
"Kwa hiyo nifunge mlango."
"Usifunge narudi sasa hivi."
***
SHARE KISHA LIKE PAGE USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA
Mustafa aliota akifanya mapenzi na Shehna huku akiahidiwa kuwa tajiri mkubwa duniani kama atampatia ujauzito. Aliposhtuka usiku alijikuta amelala sehemu ngeni machoni mwake. Ilikuwa sehemu nzuri sana ambayo hakuwahi kufika. Pembeni yake alikuwepo Shehna aliyepitiwa na usingizi.
Wote walikuwa wamelala kwenye shuka moja bila ya nguo nyingine, Mustafa alishtuka na kujiuliza ile ni ndoto au kweli. Alijaribu kujifinya ili apate ukweli alihisi maumivu, alijiuliza alikuwa wapi na alifikaje.
Ghafla alishikwa na usingizi na alipoamka alijikuta kitandani kwake akiwa amechoka sana. Alionesha alitumika usiku lakini bado alibakia njia panda kama alitumika Shehna alikuwa wapi.
Alinyanyuka na kwenda bafuni kuoga, nyumba nzima ilikuwa ikinukia manukato ya Shehna.
"Mustafa," sauti ya Shehna ilimshtua.
"Naam."
"Chai tayari," Shehna aliingia chumbani akiwa amejifunga mtandio bila nguo nyingine na kuufanya mwili wake mantashau uonekane wazi. Alimshika mkono hadi mezani kulipokuwa na kifungua kinywa kitamu kilichomfanya Mustafa amsifie.
"Hakika Mungu kakujalia kila kitu."
"Kama nini?"
"Mambo ya siri na bayana."
"Asante, nioe basi niwe mke wa pili."
"Itabidi nifanye hivyo."
"Wewee! Mkeo atakufa kwa kihoro ana wivu sana."
"Sasa itakuwaje?"
"Shida yangu kwako mtoto tu nakuacha na mama wivu wako."
Baada ya chai waliondoka pamoja kwa Mustafa kupitia hospitali na Shehna kushukia kwenye mataa ya barabarani.
"Mustafa nishushie hapa."
Mustafa alimshusha na Shehna alienda zake japo hakujua anakwenda wapi wala anakaa wapi. Alielekea moja kwa moja hospitali kumuona mkewe.Itaendelea SHARE KWA MARAFIKI NIPOST NYINGNE NASUBIRIA SHARE 250 ZIKIFIKA NDO NIPOST NYINGNE
0 comments:
Post a Comment