
Kansela wa Ujerumani Bi Angela Markel amesema kuwa, Waislamu wanaoishi
nchini humo ni miongoni mwa jamii ya wananchi wa nchi hiyo bila kujali
ni akina nani na asili yao ni wapi. Akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari akiwa pamoja na Ahmet Davutoglu Waziri Mkuu wa
Uturuki, Bi Angela Markel amesisitiza kwamba, yeye ni Kansela wa
wananchi wote wa Ujerumani bila kujadili dini na itikadi zao. Markel
amesema kuwa, anaunga mkono rai na mtazamo wa Rais wa zamani wa nchi
hiyo Christian Wulff aliyesema mwaka 2010 kwamba, Uislamu na Waislamu ni
sehemu ya Ujerumani. Kansela wa Ujerumani amesisitiza kwamba, kuna haja
ya kuweko mazungumzo baina ya dini mbalimbali. Wakati huo huo, miji
kadhaa ya Ujerumani jana ilishuhudia maandamano makubwa ya kulaani na
kupinga uenezaji chuki dhidi ya dini ya Kiislamu unaofanywa na kundi la
kufurutu ada la Pegida.
0 comments:
Post a Comment