Christiano Ronaldo atwaa tena tuzo ya mwanasoka bora wa dunia 2014

Author
Christiano Ronaldo nahodha wa timu ya taifa ya Ureno na mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid ya Uhispania ametangazwa kuwa mchezaji bora wa soka duniani kwa mwaka 2014, na kujinyakulia tuzo ya mpira wa dhahabu kwa mara ya tatu. Ronaldo ameweza kujinyakulia tuzo hiyo baada ya kuwashinda wachezaji mashuhuri duniani Lionel Messi wa Argentina anayeichezea Barcelona ya Uhispania na Manuel Neuer wa Ujerumani anayeichezea Bayern Munich ya Ujerumani. Ronaldo aliwahi kunyakua tuzo ya mchezaji bora duniani katika miaka ya 2008 na 2013.
Imeelezwa kuwa, Ronaldo ameinyakua tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa kwa timu ya taifa ya Ureno na kuipeleka kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil na mchango wake mkubwa kwa klabu yake ya Real Madrid katika kuunyakua ubingwa wa Champions League na mataji mengine mwaka jana.
Kwa upande wa wanawake, mchezaji bora wa mwaka alitangazwa Nadile Kessler, na tuzo ya goli bora la mwaka imechukuliwa na James Rodriguez wa timu ya taifa ya Colombia. Kocha wa mwaka ametangazwa, Joachim Low wa Ujerumani, na kwa upande wa kocha bora wa soka la akina dada ni Ralf Kellermann.

0 comments:

Post a Comment