#TrueStoryNo11
---------------------
SEPTEMBER 11
Na Fredy P Utd
Katika sehemu ya 10 na 11 nilionyesha ni namna gani ambavyo kuna dalili zinaonyesha kwamba inawezekana Osama bin laden na al qaida waliachwa washamiri kwa makusudi.
Pia nilionyesha ushahidi wa taarifa za kijasusi ambazo ziliwafikia serikali ya Marekani na vyombo vya usalama lakini hawakuzifanyia kazi.
Katika sehemu hii ya mwisho ningependa kujadiri dhamira ya kwanini labda Wamarekani waliacha tukio hili litokee.
Nafahamu kuwa kuna nadharia nyingi ambazo zimeenea sana kuhusu "kwanini tukio hili liliachwa litokee??"
Sasa kabla sijaanza kujadili hoja zangu, ningependa niongelee baadhi ya nadharia chache maarufu na kueleza sababu zangu kwanini siziamini hizo nadharia.
Moja; kuna nadharia kwamba hakukuwa na shambulio lolote la ndege isipokuwa zilitumika 'hologram' kuonyesha kwamba kuna ndege.
Nadharia hii ilianzishwa na Mchumi Morgan Reynolds ambaye aliwahi kufanya kazi kwenye Wizara ya Kazi kipindi cha utawala wa Bush.
Hii nadharia binafsi naiona haina mashiko kiasi kwamba haitakiwi hata kujadiliwa.
Mbili; Kuna nadharia ambayo inafanana na hiyo nadharia ya juu hapo.. Nadharia hii inapigia chapuo sana na watu wa "The Truth Movement" pamoja na manguli wa nadharia za Conspiracy, Bw. Alex Jones.
Hii nadharia inadai kuwa ndege ya flight 77 haikulipua Jengo la Pentagon bali kilicholipua lilikuwa ni Kombora (missile).
Hoja hii inatiliwa mkazo na shimo lililotengenezwa kwenye ukuta wa pentagon baada ya kulipuka. Ukiangalia lile shimo (niliwahi kuweka Picha yake, tafadhali rejea) haliendani na ukubwa wa ndege yenyewe au umbo la ndege.
Hoja nyingine ni kwamba, Jengo la Pentagon liko chini chini sana, (ghorofa tano tu) hivyo ni ngumu kwa ndege kutoka angani kujibamiza 'vertically' kwa ufanisi namna ile.
Namna pekee ingewezekana ni kwa kutumia Kombora.
Kwa haraka haraka nadharia hii inashawishi kuaminika na inaonekana ina mashiko.
Lakini, binafsi nimefanikiwa kuona kipande cha video ya Security Camera iliyokuwapo ng'ambo ya Jengo la Pentagon siku ya 9/11.
Video hii yenye urefu wa kama sekunde 6 pekee inaonyesha kwamba, kabla ya flight 77 kujibamiza Pentagon, ilikata kon a kali kuelekea Pentagon na iliruka chini chini sana kiasi kwamba bawa moja likagusa ardhini na kuvunjika.
Pia nikataka kujiridhisha kuhusu uimara wa Jengo la Pentagon. Nikakuta kwamba, Jengo hili limekuwa likifanyiwa matengenezo (renovations) tangu miaka ya 1980s.
Sasa pale pale mahala ambapo flight 77 ilijibamiza kulikuwa na 'load-bearing column' (nguzo ya kusapoti uzito wa Jengo).
Kwa hiyo bawa moja lililobakiwa lilijibamiza kwenye nguzo hii.
Hii ndio sababu kwanini likajitengeneza shimo lisilokuwa na muonekano wa umbo la ndege.
Lakini pia eneo la tukio iliokotwa miili ya watu waliokuwemo kwenye ndege, na si hivyo tu kulikuwa na makumi ya mashuhuda walioshuhudia hili likitokea (eye witness) na wakapiga 911.
Kwa hiyo hii nadharia nayo siipi nafasi.
Tatu; Kuna nadharia kwamba hakuna myahudi/muisraeli aliyekufa kwenye lile tukio kwasababu tukio lilipangwa na Israel kupitia Mosaad kwa kushirikiana na CIA.
Ajabu ni kwamba, kuna mamilioni ya watu wanaoamini hii nadharia na imejipatia umaarufu mkubwa sana pasipo watu kujua hii nadharia imetokea wapi.
Ni kwamba;
Kwa mara ya kwanza kabisa nadharia hii kuongelewa ilikuwa ni siku ya September 17 katika kituo cha televisheni cha Al-Manar nchini Lebanon.
Kituo hiki kinachorusha matangazo yake kwa Satellite kinamilikiwa na Hezbollah, wapinzani wakubwa wa Israel.
Binafsi nikisikia jambo lolote Israel wanalisema kuhusu Hezbollah huwa lazima nitie shaka kama wanasema ukweli,l.
Vivyo hivyo nikisikia chochote kinasemwa na Hezbollah kuhusu Israel lazima pia nitafakari kabla ya kukiamini.
Uhasimu wa Hezbollah na Israel umefanya hata pale muda mwingine wakiongea ukweli mtu mwingine unakuwa na mashaka, na pia wamefanya hata pale wakiongea uongo mashaiki zao wanaamini pasipo kutafakari.
Ukweli ni upi,
Mpaka kufikia leo hii tarehe 14 March 2017, imethibitika kwamba jumla ya watu 81 wenye asili ya kiyahudi walifariki katika katika tukio la 9/11.
Kati ya Wayahidi hao, watu watano wa uraia wa Israel moja kwa moja ma wengine 76 sana Uraia wa Marekani.
Hii inathibitishwa na nyaraka za wizara ya mambo ya nje ya Marekani (U.S State Department) kuhusu ripoti ya waliofariki kwenye tukio ya 9/11.
Lakini pia unaweza kutazama orodha ya majina ya waliokufa kwenye tukio la 9/11.
Lakini kwa mujibu wa taarifa za ndugu jamaa na marafiki, inakadiriwa kwamba idadi ya Watu wenye asili ya Israel/wayahudi waliokufa siku ya 9/11 inaweza kufikia watu kati ya 270 hadi 400.
Kwa hiyo hii nadharia kwamba, hakuna muisrael/myahudi aliyefariki siku ya 9/11 siipi nafasi sana.
Sasa, kwenye makala nimeeleza kuwa kuna dalili kuwa tukio liliachwa litokee kwa makusudi!!
Sasa ni dhamira gani iliwasukuma kufanya hivi??
Sasa nisingependa kutoa hoja zenye kuhitimisha huu mjadala kwa kuwa suala hili ni pana na linapaswa kuachwa lijadiliwe.. Lakini ili mjadala uweze 'kunoga' inapswa kuwe na dondoo za kusukuma mjadala mbele…
Hivyo basi, ninatoa dondoo chache za mwisho ili kuhitimisha mfululizo wa makala hizi..
'PUT OPTIONS'
Nieleze kitu Fulani kwa kifupi kabla sijaingia kwenye hoja yangu;
Katika masoko ya hisa yalioendelea kuna kitu kinaitwa 'put optionts' (au 'put/the put' kwa kifupi).
Put options ni nini?
Huu ni mkataba (ambazo ni hisa) ambapo muuzaji wa hisa (seller) anakubaliana na mnunuzi wake (buyer/holder) kwamba anamuuzia hisa lakini katika kipindi cha muda fulani mahususi (expiry/time of expiration) kama hisa hizo zitashuka thamani Fulani (strike price) basi muuzaji huyo atakuwa anawajibika kuzinunua kutoka kwa aliyemuuzia.
Tuchukue mfano rahisi;
Tuseme kwamba Fredy Utd anauza baisikeli, alafu @TheBold akaenda kuinunua baisikeli hiyo.
Lakini @TheBold anainunua hiyo baisikeli ili na yeye aweze kuiuza huko mbeleni.
Sasa tuseme labda Fredy Utd emuuzia @TheBold baisikeli hiyo kwa thamani ya 150K. Sasa ili kulinda biashara hii ya @TheBold ili naye asiingie hasara, wanasaini mkataba kwamba, labda ndani ya miezi mitatu kama ikitokea thamani ya baisikeli madukani ikishika chini ya 100K (kwafano) basi Fredy Utd atapaswa kuinunua baisikeli ile ile kutoka kwa @TheBold kwa thamani watakayokubaliana wakati wa kusaini mkataba, labda tuseme 80K (hii ndio inaitwa 'Strike Price')
Ikitokea thamani ya baisikeli haijashuka kwa kiwango kile walichokubaliana, basi baisikeli itaendelea kubaki kwa @TheBold na muda ule waliokubaliana ukipita @TheBold hawezi tena kumwambia Fredy Utd ainunue baisikeli ikitokea imeshuka thamani.
Hii ndio inaitwa 'Put Options'! Hapa nimeielezea kwa lugha nyepesi ili walau kupaga Picha, lakini ni suala pana sana.
Lakini pia papo hapo kuna kitu kinaitwa 'Call Options'.
Call option yenyewe ni kwamba, muuzaji na mnunuzi wa hisa wanakibaliana kwamba ndani ya muda fulani, ikitokea hisa zake zimefikia thamani Fulani (strike price) basi atazinunua kwa kiasi kadhaa.
Tukirejea kwenye mfano;
Tuseme Fredy Utd ana baisikeli.. Kwahiyo anaingia mkataba na @TheBold kwamba ikitokea ndani ya miezi mitatu, thamani za baisikeli zikipanda kufikia 150K basi anapaswa kuniuzia kwa shilingi kadhaa (mfano 130K) alafu namlipa hela kidogo (premium) kwa yeye kukubali kutake risk ya kuhold hiyo baisikeli (hisa) kwa muda huo.
Hii inaitwa 'Call Option'.
Sasa kwenye masoko ya hisa yalioendelea huwa wanafanya mlinganisho wa put options na call options ili kuweza kufanya 'speculation' ya mwenendo na thamani ya hisa za kampuni kwa siku zijazo.
Mlinganyo huu unaitwa, 'Put to Call Ration'.
Mfano ukifanya uwiano wa put to call ration na ukapata jawabu mfano 0.84, maana yake ni kwamba kwa kila hisa 100 zilizouzwa, hisa 84 zilikuwa ni put options na hisa 16 zilikuwa ni call options. (Hapa 'speculation' inakuwa ni kwamba hisa hizi zitadorora sana muda mfupi ujao).
Turudi kwenye mjadala,
Wiki moja kabla ya tukio la September 11 kulikuwa na mwenendo wa ajabu katika soko la hisa ambazo haujawahi kuonekana kabla.
Uchunguzi uliofanywa na Chicago Boars Options Exchange kwa amri ya kamati ya serikali ya 9/11 Commission, iligundua yafuatayo;
Siku ya September 6 na September 7 kulikuwa na 'Put Options' 4,7444 za hisa za kampuni ya ndege ya United Airline huku kukiwa na 'call options' 396 pekee.
Siku ya September 10 (siku moja kabla ya tukio) kulikuwa na 'put options' 4,516 za kampuni ya ndege ya American Airlines huku kukiwa na 'call options' 748 pekee.
Kumbuka kwamba kampuni hizi mbili ndizo ndege zake zilihusika katika ulipuaji majengo.
Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba 'trend' hii haikuonekana kwenye hisa za kampuni nyingine za ndege.
Hii ilimaanisha kwamba, 'Traders' katika masoko ya hisa walikuwa wamepenyezewa taarifa kwamba ndani ya siku chache kuna tukio litatokea na kufanya hisa za kampuni za American Airlines na United Airlines zishuke.
Kwahiyo traders wakatumia hiyo fursa kucheza na mahesabu ya 'put to call ratio' kujitengenezea faida ya mabilioni ya dola.
Si hivyo tu;
Hili pia lilitokea kwenye kampuni ya bima ya Citygroup Inc. kupitia 'package' yao ya Traveller Insurance.
Hawa walikuwa na mikataba ya kulipa fidia ya zaidi ya shilingi Trilioni moja (fedha za kitanzania) kwa makampuni wateja wao yaliyopo kwenye Jengo la WTC ikiwa litatokea shambulizi kwenye jengo hilo.
Pia hawa katika soko la hisa walikuwa wanalipa 'put options' ikitokea thamani ya hisa zimeshuka chini ya dola 40 kwa dola moja.
Siku tatu kabla ya shambulio kulitokuwa na 'put option' za kiwango cha juu ambazo hazijawahi kushuhidiwa kwenye hisa ya kampuni hiyo. Put options zilikuwa ni mara 45 kuzidi siku zao za kawaida.
Haikuishia hapo tu......
0 comments:
Post a Comment