#TrueStoryNo9
---------------
SEPTEMBER 11
Na Fredy P. Utd
CRASHING
Katika sehemu ya nane nilieleza kuhusu namna ambavyo "vitivo" viliwasili uwanja was ndege, walivyopanda kwenye ndege na hatimaye kuziteka..
Kwenye sehemu hii ya 9 nitazungumza namna ambavyo ndege hizo zilivyobamizwa kwenye targets..
Tuendelee..
Kitivo cha Town Planning (Flight 11)
Baada ya waongozaji ndege ardhini kugundua kuwa flight 11 imedhibitiwa na watakaji, moja kwa moja saa 08:37 AM wakawasiliana na Northeast Air Defense Sector (NEADS) jijini New York.
NEADS wakawasiliana na kituo cha kijeshi la Anga, Otis Air Force Base kilichopo Mashpee, Massachusetts, kuomba ndege ya kivita ya F-15 kuifutilia Flight 11 na ikiwezekana kuidungua.
Baada ya mawasiliano hayo kufanyika, ndege ya kijeshi F-15 ilikuwa tayari huku ikisubiri ruhusa ya kupaa na kuanza kuifuatilia Flight 11.
Saa 08:43 AM flight 11 ilikata kona ya mwisho kuingia New York eneo la Lower Manhattan.
Saa 08:46 AM ruhusu ilitolewa kwa ndege ya kijeshi F-15 kuruka kuifuatilia flight 11 (iliruka saa 08:53 AM).
Wakati ambao F-15 inapewa ruhusa ya kuruka saa 08:46 AM, tayari Mohamed Atta alikuwa amefikisha flight 11 kwenye target..
Kwahiyo muda huo wa saa 08:46 AM, flight 11 ikiwa na abiria 81 na wahudumu 5 na ikiwa kwenye mwendo wa kilomita 748 kwa saa, na kwenye tank la mafuta ikiwa na Lita 38,000 ya mafuta… flight 11 ilibamizwa na Mohamed Atta kwenye North Tower ya World Trade Center katikati ya ghorofa ya 93 na 99.
Iliua abiria wote ndani ya ndege na mamia wengine waliomo kwenye jengo.
Miongoji mwa abiriia walikufa alikuwemo Mtengenezaji wa kipindi cha televisheni cha Frasier, Bw. David Angell na mkewe Lynn Angell. Pia alikuwemo muigizaji Berry Berenson na Mtunzi wa 'Family Guy', Bw. Seth MacFarkine.
Kitivo cha Town Planning II (flight 175)
Nilieleza namna ambavyo Al-Shehhi na wenzake wa Kitivo hiki waliiteka na kuidhibiti hii ndege.
Saa 9:01AM flight ikaanza kwenda kwa kasi kushuka kwenye eneo la Lower Manhattan.
Saa 09:03 sekunde ya 2, flighg 175 kwa muelekeo ilikuwa inaonekana kana kwamba itajibamiza kwenye jengo la 'Empire State' lakini ilikata kona kali ghafla na kwenda kujibamiza kwenye South Tower ya World Trade Center kwa kasi ya kilomita 950 kwa saa ikilipua Lita 38,000 pia zilizokuwamo kwenye tank na kuua abiria wote 56 na wahudumu 9 waliokuwamo kwenye ndege na mamia wengine waliokuwemo kwenye jengo.
Flight 175 ikiendeshwa na Marwan al-Shehhi ikikaribia kujibamiza South Tower ya WTC huku pembeni North Tower ikiendelea kuteketea baada ya kulipuliwa na flight 11 iliyoendeshwa na Mohamed Atta.
Kitivo cha Fine Arts (flight 77)
(Nilieleza pia namna ilivyotekwa na Hani Njour na Kitivo chake)
Baada ya kukaribia kabisa ofisi za Pentagon, Hani inakadiriwa kuwa alikatisha kona ndege kwa nyuzi 330 kuelekea upande wa magharibi mwa Pentagon na kusafiri mita 670 kutoka juu angani kushuka chini.
Saa 09:37 AM Hani Njour aliibamiza ndege upande wa magharibi mwa Pentagon (west wing) gjorofa ya kwanza, kwa kasi ya kilomita 853 kwa saa.
Kitivo cha Law (flight 93)
(Nilieleza pia namna walivyoidhibiti)
Baada ya Ziad Jarrah na wenzake kufanikiwa kuingia kwenye chumba cha marubani inasemekana kuwa waliwajeruhi marubani na kuanza kuiondoa ndege kwenye njia yake.
Baada ya hapo; Ziad Jarrah akatoa tangazo kwa abiria, akawaambia;
"..ladies and gentlemen. Here the Captain. Please sit down. Keep quite…"
(sikiliza audio ya sauti ya Jarrah hapo chini)
Saa 09:35AM sekunde ya 09 Ziad Jarrah akinua ndege juu mpaka kufikia umbali wa mita 12,400.
Hii iliwafanya waongozaji wa ndege kuondoa ndege nyingine zote kutoka kwenye njia hiyo.
Saa 09:39 AM Ziad Jarrah akatoa tangazo lingine kwa abiria, akiwaambia;
"..here is the Captain. I would like to tell you all to remain seated. We have a bomb, and we are going back to the airport, and we have our demands. SK please remain quite.."
(Sikiliza audio ya sauti ya Jarrah hapo chini)
Kutokana na kitivo hiki kuwa pungufu ya mtu mmoja tofauti na mkakati wao walioupanga awali (kumbuka al-qahatani aliyerudishwa airport), hivyo iliwabidi wawarudishe abiria nyuma ya ndege na kufunga milango kuingia 'business class' na chumba cha rubani.
Kutokana na abiria kuachwa peke yao nyuma ya ndege hii iliwafanya kuwa huru kufanya mawasiliano wa watu ardhini.
Jumla ya simu 35 zilipigwa kutoka kwenye ndege kwenda chini ardhini.
Moja wapo ya simu hizo za majonzi makubwa ilipigwa saa 09:47AM sekunde ya 57 ambayo ilipigwa na muhudumu wa ndege aliyeitwa CeeCee Lyles ambayo alimpigia mumewe ambayo hakuwa karibu ma simu na ikambidi aache ujumbe wa sauti (voicemail).
(Sikiliza audio chini)
Saa 09:57 AM abiria aliyeitwa Tom Burnett aliwaongoza abiria wenzake kufanya 'Mapinduzi' ili kuiweka ndege kwenye udhibiti wao.
Hivyo wakaanza kutimia nguvu kwa pamoja kubomoa mlango wa business Class na hatimaye kuanza kubomoa mlango wa chumba cha marubani.
Saa 09:59 sekunde ya 52 Ziad Jarrah aligundua juu ya nia ya 'mapinduzi' hayo yanayotaka kufanywa na abiria, kwahiyo akaanza kuendesha ndege kama anaibiribgisha (roll) ilikuwafanya abiria wakose 'balance' ya kusimama na kuwajeruhi.
Saa 10:00AM sekunde ya 03 Ziad Jarrah akaituliza ndege.
Baada ya kuituliza licha ya abiria wengi kuwa wamejeruhiwa lakini wakaanza tena harakati za kuingia kwenye chumba cha marubani.
Baada kidogo zinasikika sauti za Jarrah na wenzake wakishauriana kuidondosha ndege kabla ya kuifikia target (whitehouse) ili kuepuka ndege kudhibitiwa na abiria na kutua chini salama.
Saa 10:01AM sekunde 00 Ziad Jarrah ma wenzake wanasikika wakipiga "Takbir.!"
Saa 10:03 AM sekunde 01 Ziad Jarrah akiendesha ndege kwa kasi ya kilomita 906 kwa saa aliendesha ndege kwa nyuzi 40 kuelekea chini na kuidondosha kwenye eneo la Shanksville, Pennsylvania na kuua abiria wote 37 na wahudumu 7 waliokuwemo ndani ya ndege.
West wing ya Pentagon ikiwa imeteketea na kuharibika vibaya baada ya kulipuliwa na flight 77 iliyoendeshwa na Hani Hanjour.
Zimamoto, wahudumu wa dharura na raia wakifanya uokoaji baada ya maghorofa ya WTC kudondoka baada ya kuwaka moto kwa takribani dakika 102.
'Blank' Reaction
Katika moja ya vitu ambavyo bado vinabishaniwa sana kwenye nyanja ya usalama na saikolojia ni 'reaction' ya Rais George W. Bush Mara baada ya kueleza hili tukio nililolieleza..
Siku hii ya 9/11 Rais Bush alikuwa ametembelea kwenye Shule ya Awali ya Ema E. Booker Elementary School iliyopo Sarasota Florida.
Katika moja ya shughuli ambazo alizifanya shuleni hapo ilikuawa ni kuwasomea wanafunzi kitabu cha "The Pet Goat" (kitabu hiki pia kilitajwa na Bin Laden kwenye video yake iliyosambaa sana kwa wanachama wa al-qaida mwaka 2004 (nitaeleza hii "coincidence" huko mbeleni)).
Aliwasomea watoto kitabu kwa dakika 13 kabla ya kuja kunong'onezwa jambo na Katibu Mkuu kiongozi wa Ikulu Bwana Andy Card.
Jambo ambalo Andy Card alimnongoneza Rais Bush ilikuwa ni taarifa kuwa kuna shambulio kubwa la ugaidi limefanyika kwenye ardhi ya Marekani..
Ajabu ni kwamba Bush hakuonyesha reaction yoyote (tazama Picha tena)
Hakukasirika, hakustuka, hakucheka wala kuchukia.. Reaction yake ilikuwa ni "blank".
Na ajabu zaidi akaendelea kuwasomea watoto kitabu kwa dakika saba zaidi (jumla dakika 20).
Baada ya hapo Maafisa wa Secret Service wakamuondoa na kufanya darasa moja kama ofisi ya dharura ili Bush aweze kupewa briefing kutoka vyombo vya usalama
Rais George W. Bush akiwasomea wanafunzi kitabu siku ya 9/11 katika shule ya Emma E. Booker.
Katibu kiongozi Andy Cardy akimnong'oneza Rais kuhusu shambulio linaloendelea.. (tazama facial expresion.. iko neutral.. 'blank')
Katika sehemu ya hizi Tisa za mfululizo wa makala hizi kuhusu 9/11 nimemaliza kueleza namna ambavyo tukio la 9/11 lilipangwa na kutekelezwa… niliahidi kuendeleza sehemu zitakazo fuata kwa kuangalia upande wa pili wa suala hili kwa kuyaangazia masuala yenye utata.
Sasa basi,
Yako maneno mengi na nadharia nyingi sana zinazo jaribu kueleza utata wa suala hili.
Kwa mfano, hiko nadharia isiyo na ushahidi wowote (lakini ajabu inaaminiwa na wengi) kwamba Bin Laden na Al-Qaida "wamesingiziwa" kuhusika na tukio lile. Labda hii inapewa nguvu zaidi kutokana na misimamo ya kiimani na kiitikadi, lakini binafsi sio mfuasi wa hili nadharia ya "kusingiziwa" Osama kuhusika na shambulio.
Lakini hii haiondoa uhalisia kwamba kuna mambo mengi mazito yenye kutia shaka kuhusu kufanikiwa kwa shambulio la 9/11.
Kuelewa kwa ufasaha utata huu, inapasa kufukunyua kwa kina taarifa za siri kutoka IC (Intelligence Community) za Idara mbali mbali nchini Marekani.
Katika mjadala wangu nitaangazia masuala haya yenye utata kwa katika milengo ya nadharia za dizaini mbili kuonyesha nini kilikuwa kinaendelea kwenye IC.
Misingi ya nadharia hizi ni zifuatazo;
1. LIHOP (Let It Happen On Purpose)
Nitaeleza dalili zinazoonyesha kuwa kulikuwa na watu waandamizi kwenye Serikali ya Marekani waliokuwa na ufahamu juu ya kinachoendelea lakini kwa makusudi wakapuuzia au kudhoofisha utendaji wa vyombo vya usalama kukabiliana na hatari.
2. MIHOP (Make It Happen On Purpose)
Nitaeleza dalili za baadhi ya watu waandamizi ambao zinaonyesha kuwa walipanga au kushiriki au kuwasaidia magaidi kufanikisha tukio lile.
HUSIKOSE #TrueeStoryNo10 hapo kesho tena... 😂😂😂
#TheBold
Keep up the good work mateHere For more Extraordinary enlightening post
ReplyDelete