SEPTEMBER 11

Author

#TrueStoryNo2
---------------
SEPTEMBER 11

Na Fredy P. Utd

OSAMA ATIRIRISHA FATWA
Mwanzao kabisa baada ya Al Qa'ida kuundwa mwaka 1988 ilitokea sintofahamu katika uongozi wake wa juu ambapo Osama na Azzam wakatofautiana kuhusu mkakati wa namna ya kupambana na adui yao mpya Marekani na nchi za magharibi.

Osama alipendekeza kuwa Al Qa'ida ijikite zaidi katika mashambulio ya kujitoa muhanga pamoja na mashambulio yenye kulenga minundombinu na maeneo ambayo yana wamarekani au wazungu wengine.

Azzam hakukubaliana na hili na akatumia ujuzi wake wa elimu ya dini na ushawishi wake kusambaza ujumbe (fa'twa) yenye kupinga mashambulio ya kujitoa muhanga au kushambulia maeneo yenye mikusanyiko ya watu akidai kuwa mashambulio hayo yanaweza kusababisha vifo vya watoto na wanawake kinyume na dini ya kiislamu inavyokataza kuua wanawake na watoto katika vita.

Hii ilifanya mahusiano ya 'kikazi' na 'kiitikadi' kuzorota kati ya Osama na swahiba wake Azzam.

Novemba 1989 Abdullah Azzam akiwa na familia yake kwenye gari akielekea kwenye swala ya ijumaa eneo la Peshwar nchini Pakistani waliuwawa kwa bomu ambalo lilikuwa limetegwa barabarani..

Mpaka leo hii kuna utata mkubwa juu ya wahusika wa kifo cha Abdullah Azzam.
Wengine wakidai Mosaad ilihusika ili iweze kumfunga mdomo kutokana na msimamo wake mkali wa kupinga Israel kudhibiti eneo la Palestina.

Wengine wanaihisisha CIA na kifo cha Azzam.
Lakini katika ulimwengu wa masuala ya Intelijensia, wengi wanaamini Osama bin Laden yuko nyuma ya kifo cha "mwanazuoni nguli" Abdllah Azzam, Father of Global Jihad.

Vyovyote vile ukweli ulivyo, lakini kifo cha Azzam kilipandisha zaidi 'status' ya Osama ndani ya Al Qaida na vikundi vya Mujahedeen kwa kuwa sasa hakukuwa na mwanafalsafa wa kupinga mikakati yake.

MAANDALIZI YA AWALI

Mwaka 1991, Osama bin Laden alihmishia makazi yake nchini Sudan akiongoza wapiganaji wake kufanya mashambulio ya ukubwa wa kati mfano, shambulio dhidi ya msafara wa wanajeshi wa Kimarekana mjini Mogadishu mwaka 1993.
Mwaka 1996 alihamishia tena makazi yake nchini Afghanistan.

Fa'twa ya kwanza

Fa'twa ya kwanza kutolewa na Osama ilikuwa ni mwaka 1996 na ilikuwa na ujumbe wa moja kwa moja.

Kwanza aliwataka waislamu hasa waliojitoa kwa ajili ya dini ya kiislamu kupinga umagharibi na desturi zao. Lakini pia akaitaka Marekani kuondoa vikosi vyao vya kijeshi vilivyopo Saudi Arabia akisisitiza kuwa ardhi hiyo ni takatifu si sahihi kuwepo kwa majeshi ya "kafir".

Fatwa hii ilijipatia umaarufu sana katika 'ulimwengu' wa vikundi vya kigaidi na iliwavutia wengi.

Moja ya waliovutiwa kwa kiwango kikubwa na fa'twa hii alikuwa ni Khalid Sheikh Mohammed maarufu kama KSM ambaye kwa miaka mingi amwkuwa akitamani kukutana na Osama.

Khalid Sheikh Mohammed ni nani??

Msomi wa Shahada ya Sayansi ya Uhandisi (Bachelor of Science in Mechanical Engineering) aliyoipata kutoka Chuo kikuu cha Chowan, jimboni North Carolina nchini Marekani.
Amezaliwa tarehe 14 April 1965 eneo la Bacholistan, nchini Pakistan.

Akiwa na miaka 16 pekee aliwahi kusikia mahubiri ya mwanatheolojia wa kiislamu aliyeitwa Abdul Rasul Sayyef na alivutiwa sana na mahubiri hayo yaliyohusu Jihad.

Baadae ndio akaenda kusoma nchini Marekani. Taarifa za intelijensia zinaamini kuwa kitendo cha KSM kuishi Marekani kulimfanya aichukiw zaidi nchi hiyo badala ya kuipenda au kupunguza msimamo wake mkali.

Moja ya matukio yaliyomfanya kuichukua zaidi Marekani ni kitendo cha kuwekwa jela kwa muda kutokana na kushindwa bili zake.

Baada ya kumaliza chuo, mwaka uliofuata yaani 1987 yeye na kaka yake wakaelekea Afghanistani kujiunga na vikundi vya Mujahedeen.

Baada ya vita na majeshi ya Urusi kuisha mwaka 1989 KSM akaendelea kujihusisha na mitandao ya kigaidi akitumia muda wake mwingi kuishi nchini Qatar kama muhandisi akitumia majina ya bandia.

Baadae kati ya mwaka 1993 na 1995 akaelekea nchini ufilipino ili kutekeleza mpango wa Kigaidi dhidi ya Marekani.

Yeye na wenzake watano wakapanga kuwa wachague siku maalumu ambayo watakuwa wakipanda ndege zaidi ya kumi na mbili za abiria za kimarekani (wanapanda na kushuka kabla ya ndege kuruka) lakini ndani ya ndege kwenye mizigo kwa ustadi mkubw watakuwa wanaacha mabegi yenye mabomu yaliyotegwa kulipuka kwa muda maalumu.

Wakachagua ndege za 'kuzitarget', na wakachagua siku watakayo Fanya hivyo.

Kabla ya tukio lenyewe kwanza wakaona wajaribu kwenye ndege binfsi ya mtu ili waone 'impact' yake

Hapa ndipo wakaharibu mpango wao, kwani walifanikiwa kutega bomu kwenye ndege ya mtu na ndege iliporuka wakailupua na rubani wa kijapani aliyekuwemo kwenye ndege akauwawa.

Hii ikapelekea kufanyika uchunguzi mkali wa vikosi vya ufilipino kwa kusaidiwa na CIA na hatimaye wakagundua mkakati wa KSM na wenzake.

Baada ya mkakati kugunduliwa ikambidi KSM kukimbia na kurudi Qatar, lakini nako tayari taarifa zake zilikuwa zimefika kuwa anatafutwa na marekani na ndipo hapa ikambidi akimbilie Afghanistani.

Kipindi hiki ambapo KSM alikimbilia Afghanistan ilikuwa ni mwaka 1996 na ndio kipindi hiki ambapo Osama Bin Laden alitoa fa'twa yake ya kwanza ambayo ilimvutia sana KSM na akaanza tena mikakati aweze kuoanana na Osama.

Ikanbidi atumie connections zake zote alizonazo kwenye mitandao ya kigaidi na hatimaye akafanikiwa kukuatana na moja ya maluteni wakuu wa Al Qaida aliyeitwa Mohammed Atef.

Baada ya kumueleza Atef kuhusu nia yake ya kutaka kuonana na Osama, Atef akakubaliana naye na kati kati ya mwaka 1996 Mohammed Atef akaandaa kikao maakumu katika milima ya Tora Bora kati ya Osama Bin Laden na Khalid Sheikh Mohammed.

Ni katika kikao hiki ambapo KSM aliwasilisha mkakati ambao ulitumika kutekeleza tukio la September 11.

Siku hii ambayo KSM alionana na Osama akiwa pamoja na Mohammed Atef moja ya makamanda wakuu wa wapiganaji wa All Qaida.. KSM akawasilisha mpango unaofanana kabisa na ule mpango ambao alidhamiria autekeleze nchini Ufilipino.

KSM alimuelezea bin Laden namna ambavyo mkakati huu utatekelezwa hatua kwa hatua.

Mkakati huu (KSM alivyoueleza kwa Osama mwaka 1996) ulihusisha namna ambavyo wataweza kupenyeza wapiganaji wa Al Qaida nchini marekani na namna ambavyo watateka jumla ya ndege kumi na mbili kutoka pwani ya Mashariki ya Marekani na pwani ya Magharibi.

KSM akapendekeza ndege hizi zikishatekwa ziende zikababizwe na kujilipua katika majengo yafuatayo;

- World Trade Center, New York City

- The Pentagon, Arlington, Virginia

- The Prudential Tower, Boston, Massachusetts

- The Whitehouse, Washington, DC.

- The Willis Tower (The Sears Tower) Chicago, Illinois

- The U.S Bank Tower, Los Angels, California

- Transamerica Pyramid, San Fransisco, California

- Columbia Center, Seattle, Washington

Hizi ndizo zilikuwa original targets ambazo zilipendekezwa na KSM katika kikao hiki na Osama.

Osama alikubaliana na mapendekezo ya hizi targets isipokuwa tu Jengo la U.S Bank Tower akataka liondolewe kwenye orodha (nitaeleza mwishoni mwa makala nadharia za intelijensia zinazo jaribu kufafanua uamuzi huu wa 'utata' kwa Osama kutaka U.S Bank Tower iondolewe kwenye orodha).

Lakini kwa ujumla wake Osama akaukubali mpango wote wa KSM na akamuomba KSM ajiunge rasmi na kuwa mwanachama wa Al Qaida.

Ilichukua miezi kadhaa (na wengine wanadai mwaka mzima) kumshawishi KSM kuwa mwanachama wa All Qaida.. Yaani KSM alikuwa ni muamini katika masuala ya ugaidi lakini alikuwa anapenda abaki kuwa huru asijifunge nankikundi chochote.!! Lakini mwishowe akakubali kujiunga na kuwa mwanachama rasmi.

Hivyo basi mwaka uliofuata 1997 KSM akaihamisha familia yake iliyokwepo Iran na kuipeleka Karachi, nchini Pakistan ili awenayo karibu yeye mwenyewe akielekea Kandahar katika harakati zake nchini Afghanistan.

Mara ya kwanza alipoingia kuwa mwanachama wa Al Qaida, KSM alipewa uenyekiti wa kamati ya habari (media committee) lakini baadae akapendishwa cheo mpaka kupewa uenyekiti wa kamati ya kijeshi. (Military Committee).

Kazi kubwa ya KSM katika kipindi hiki ilikuwa ni kukusanya taarifa za intelijensia za kutosha kuhusu Marekani na kufanya vetting' ya vijana ambao wana potential ya kuweza kutumika katika tukio hili kubwa zaidi kuwahi kupangwa na Al Qaida....

Husikose kesho #TrueStoryNo3...

#TheBold

0 comments:

Post a Comment