"Jamanimpenzi njoo hii sikukuu ya wapendanao tuwe sote" Miriam alimpigia mumewe simu kumsihi arudi Arusha ili siku ya tarehe 14 mwezi wa pili wawe pamoja.Genes alijitetea kubanwa na kazi hivyo hakufanikiwa kurudi Arusha lakini lengo lake likiwa ni kuzunguka na. Angel pamoja na watoto wake.Wakiwa katika matembezi na gari aina ya Toyota Corolla,Genes alikua usukani Angel akiwa pembeni yake na watoto wakiwa nafasiza nyuma,gari ilikua inatembea kasi na ghafla walipata ajali iliyosababishwa na lori kupoteza mwelekeo na kigongana uso kwa uso.Genes na Angel walifia hapo hapo.Taarifa zilisambaa kwa harakahadi zilifika kwa Miriam.Ilikua siku yakilio kikubwa sana kwani hakuamini kama mwanaume aliyempenda hivyo ameaga dunia tena ghafla.Alitoka na kufuatilia mwili na ndipo alipopata maelezo juu ya ajali na watoto waliokua katika gari hiyo baada ya kufuatilia aligundua watoto hao ni mapacha na wapo hai katika matibabu.Mipango ya mazishi ilifanyika na Genes alisafirishwa hadi nyumbani kwao Arusha.Baada ya wiki tatu Miriam alifuatilia wale watoto ili kujua walikua wametoka wapina ndipoalipata ukweli wote juu ya hao watoto na huyo mwanamke aliyekufa na mumewe."basi kama nyie ni watoto wa Genes aliyezaa na Angel basi nitawatunza kama wanangu" Miriam aliwaambia na kuwa pakia katika gari na kurudi nao Arusha, ali wasomesha na kuwapa mahitaji muhimu.Miriam kuanzia siku hiyo haku shughulika na masuala ya mapenzi kwani aliamini kama asinge jiingiza kwenye masuala ya mapenzi basi asingelia katika maisha yake.Baada ya sifa zake kuzidi kuenea nchi nzima basi wazazi wake walitafutwa na kukutanishwa na mwanaye,walifanya sherehe kubwa na Miriam mbeleya wanafamilia ali ahidi kua watoto
wa takao rithi mali zake ni Eledy na Eledius
Mwisho
0 comments:
Post a Comment