Hotuba fupi ya Mh Lowassa Kilolo - Iringa Leo hii.
KUHUSU KUWASHUKURU WANANCHI.
Moja nimekuja kuwashukuru na kuwaeleza tulishinda na ndio maana hawa mabwana wakubwa wanapata tabu sana Na Mimi , nilitangaza kuanza ziara ya kushukuru wananchi kwa hizo kura milioni 6 wakazuia mikutano ya hadhara haitoshi wakazuia mikutano ya ndani pia ninayotaka kuhudhuria ,wanatisha wafanyabiashara wanatukodisha kumbi za mikutano wanateseka kweli kweli.
CHADEMA chama chetu ni kikubwa sana , kinawatesa sana , tumewachapa kweli kweli uchaguzi Mkuu 2015, tumewashinda katika majiji na miji mikuu kiasi wanapata Tabu kweli kweli , wageni toka Nje wakija pale Airport Rais huwa anaulizwa kuhusu mameya wetu na anapata kigugumizi kutambulisha kuwa hawa ni wapinzani .
Pili Uchaguzi Mkuu ujayo 2020 tutashinda tukiwa wamoja , tuwe wamoja na wanajua sisi ni wamoja . Mkutano mkuu CCM kule Dodoma walinitaja Mara 360 na zaidi , mkutano ule ulikuwa wa Lowassa kwa kuwa wanateshwa na jinamizi langu , linawatesa kweli kweli , kule nimetoka na CCM haipo tena nimeacha Lowassa na ndio sababu wanapata tabu kwa kuwa wanajua tumewashinda nchi hadi ndani ya chama chao.
KUHUSU UKUTA .
Jambo hili la UKUTA ni kubwa mno si jambo dogo hata kidogo ,Jana balozi wa Marekani aliwatumia ujumbe raia wake wajiandae kuondoka tarehe 1 September kwa hofu walionayo. Hata Mimi nina hofu kama tusipotekeleza hili nchi itakuwa wapi hapo baadae. Haiwezekani mtu mmoja ajiamulie tuu kila jambo na kuvunja katiba .
Wasuluhishi wanasema tuzungumze , tunakubali kuzungumza ,lakini tuzungumze nini ikiwa mtu anavunja Katiba na hawamuonyi hawamshauri hii si sawa kabisa. Mtu mmoja anajiamulia kuvunja katiba anazuia mikutano anazuia mikutano ya ndani na wasuluhishi hawamuonyi ,nasema kabla ya kuja kwetu wakamueleze yeye kwanza matendo yake .
POLISI niwaeleze duniani kote maandamano ni haki ya msingi kabisa , police wakiua raia au wanachama wetu tuwaarifu dhahiri tutadeal nao mmoja mmoja, hatutodili na jeshi tutadili Na Polisi aliefanya mauaji, alie fyatua risasi ajue dhahiri tutamshitaki ICC . Ni bora tufilisike ,tutaabike lakini tutawalinda watanzania Na waandamanaji wetu wote nchi nzima Kata zote kama tulivyo kubaliana.
Tabia za viongozi Wa kiafrika ni mbovu sana , wanavunja Katiba Na kukanyaga demokrasia , hili hatuwezi kuliruhusu litokee hata kidogo litokee Tanzania. Zipo jitihada za usuluhishi hatuna shaka nazo lakini wajue jambo tunalolipigania liko wazi ni Katiba wamwambie aruhusu mikutano na haki za kidemokrasia .
Tujitokeze kwa wingi sana September 1, tuandamane bila kuharibu Mali ya mtu kama tulivyofanya wakati Wa kuchukua Fomu pale buguruni ,Tume hadi Kinondoni bila hofu . tuna chama Imara sana CHADEMA kinacho tetea Uhuru ,haki ya mwananchi , maendeleo na ustawi wa nchi . Tunawapenda sana, ninawapenda Na Ahsanteni kwa kunisikiliza.

posted from Bloggeroid
0 comments:
Post a Comment