MUUNGANO MPYA WA KIBIASHARA AFRIKA

Author
Jumuya tatu za kikanda zinajiandaa kuungana kuunda soko huru kubwa barani Afrika. Leo jumuya ya maendeleo kusini mwa Afrika, jumuya ya Afrika Mashariki na COMESA, zinatarajiwa kusaini mikataba ambayo itaruhusu uanzishwaji rasmi wa muungano mpya.
Inakisiwa kuwa mpaka kufikia mwa 2017, zaidi ya Waafrika million mia sita watafaidika na mpango huu. Mkutano wa maafisa wa biashara nchini Misri unaendelea huku wakiwa katika hali ya mashaka kukamilisha mpango huo.
Inaarifiwa kuwa mpango huo utakuwa tayari kusainiwa hii leo. Baada ya hapo, mapatano hayo yatazinduliwa rasmi kwenye mkutano wa umoja wa Afrika mwishoni mwa juma hili.
Baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, jumuya ya kibiashara ya Afrika itaanzisha soko moja kubwa la pamoja litakalohusisha nchi ishirini na sita.
Lengo la jitihada hizo ni kuondoa vikwazo katika bidhaa ambapo itakuza shughuli za kiuchumi zenye thamani ya kiasi cha dola za kimarekani trilion moja.
Kukamilika kwa mpango huu huko Sharma Sheikh nchini Misri itakuwa ni hatua ya awali tu, baada ya hapo mkataba huo utahitajika kuhakikiwa na bunge la kila nchi, kabla ya kuanza rasmi kufanya kazi.
Muungano kwa Afika si jambo jipya. Takribani nusu karne tangu Bara la Afrika lilipojipatia uhuru, serikali zimekuwa zikijadili namna ya kukuza biashara ya ndani.
Miundombinu mibaya kama vile reli, barabara na usafiri wa anga ambapo inaleta ugumu kupitisha bidhaa mipakani. Pia nchi nyingi zinajaribu kulinda viwanda vyao vya ndani.

0 comments:

Post a Comment