Selina alifariki Februari 2, katika Hospitali
Teule ya Wilaya ya Nyerere baada ya kuugua kwa muda mrefu na kuzikwa
Februari 3, mwaka huu kijijini hapo na Machi 22 ikiwa ni siku 20
walikuta kaburi limefukuliwa sehemu ya kichwani na miguuni. Hivyo kutoa
taarifa polisi ili kupata kibali cha mahakama kufukua na kuhakiki
kilichomo.
Ufukuaji huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Serikali
ya kijiji hicho, Mtiro Marinya chini ya maelekezo ya wazee wa mila ya
jamii ya Kiikoma. Zoezi hilo lilitawaliwa na usiri mkubwa baada ya
kubaini sehemu za siri, vidole vya mguu na sikio la kushoto
vimenyofolewa.
Katibu wa mila ya jamii ya Waikoma, Hussein
Ramadhani mmoja wa waliohusika kwenye zoezi la ufukuaji alisema kwamba
walipobaini vitendo visivyo vya kawaida kwa ushauri wa wazee
walikubaliana kutokuwaambia wanawake ili kupunguza hofu lakini
kilichofanywa kinahusishwa na imani za kishirikina.
“Vitendo hivi ni vya kishirikina maana kufukua
kaburi na kukata viungo hivyo kisha kufukia haya ni mambo ya kishirikina
zaidi...Hali kama hii ukiisema hadharani utazua hofu na ndiyo maana
wanawake wameruhusiwa kuangalia kama ni yeye ama la walioweza wameona,”
alisema.
Naye Mzee wa Mila, Nyarancha Kichembu kutoka
Kijiji cha Bwitengi alisema, tukio hilo ni la kwanza kutokea na kuwa
wanawake hawapaswi kuambiwa hali halisi na kuwa limewasikitisha na
linawapa wakati mgumu kutafuta undani wa vitendo hivyo.
“Kama maiti isingelikutwa ndani angenyongwa kondoo
jike na kutumbukizwa ndani na kuzikwa kisha taratibu za kimila
zingefuata maana si mambo ya kawaida haya….lakini kwa hili
lililojitokeza uchunguzi unaendelea ili kubaini wanaojihuisha na vitendo
hivyo vinavyozidisha hofu kwa watu,” alisema.
Mama mzazi wa marehemu huyo Nyahande Kwimambo
alisema “Kuna kitu kisicho cha kawaida kilitokea Machi 22 kwa kawaida
tunaamka saa 12 alfajiri lakini siku hiyo tuliamka wote saa nne na
kukuta kaburi limefukuliwa sehemu ya kichwa na miguuni, ikabidi nipige
yowe,” alisema.
Alibainisha kuwa hofu yake ilikuwa ni kwamba
mwanaye alichukuliwa, lakini baada ya kufukua ameona kuwa ni yeye roho
yake imetulia, hata hivyo waliohusika na kufukua hawakumweleza
walichobaini baada yake walimtaka athibitishe kama ndiye kisha wakazika.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Marinya
Marwa alisema walifikia uamuzi wa kufukua baada ya hofu kutanda kijijini
hapo na kuwa taratibu zote za kisheria zimefuatwa na hivyo walichoona
watu, yeye hawezi kuyasemea zaidi mambo hayo na kuwa watatoa taarifa kwa
vyombo husika






0 comments:
Post a Comment