LIVERPOOL YA SONGA MBELE

Author
Liverpool wamefanikiwa kusonge mbele na kutinga kwenye hatua ya nusu fainali kwa kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri lililofungwa na kiungo mshambuliaji kutoka nchini Brazil, Philippe Coutinho Correia.
Kwa matokeo hayo, Liverpool watacheza dhidi ya Aston Villa katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kombe la FA utakaounguruma kwenye uwanja wa Wembely April 19, kwa kutanguliwa na mchezo kati ya Reading dhidi ya Arsenal utakaopigwa April 18.

WAKATI HUO HUO

Mshambuliaji kutoka nchini Italia Super Mario Barwuah Balotelli amedhirisha hadharani hali yake ya kimwili baada ya kukosekana kwenye kikosi cha Liverpool wakati wa mchezo wa hatua ra robo fainali uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo huko Ewood Park dhidi ya Blackburn Rovers.
Balotelli amedhihirisha hadharani hali yake ya kimwili kutokana na maswali mengi kuzizima miongoni mwa mashabiki wa klabu ya Liverpool ambapo baadhi yao waliamini huenda alikua na matatizo binafsi.
Balotelli ameonyesha kusikia malalamiko ya mashabiki hao kwa kupiga picha na kuiweka kwenye mitandao ya kijamii ambayo inaonyesha majibu ya kipimo cha joto la mwili wake ambacho kinasomeka nyuzi joto 38.7.

0 comments:

Post a Comment