Taarifa ya ACT iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa
ziara hiyo ya siku 10 inaanza leo mkoani Ruvuma na itamalizika Aprili
19, mkoani Mara.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa baada ya Ruvuma ACT itaelekea Njombe,
Iringa, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza na kisha
Mara.
Chama hicho kimeanza harakati za kujitangaza siku chache baada ya
kuzinduliwa rasmi na baada ya aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini
(Chadema), Zitto Kabwe, kujiuzulu ubunge na kujiunga nacho.
Zitto ambaye ndiye msemaji mkuu wa ACT-Tanzania alijiunga rasmi na
chama hicho Machi 21, mwaka huu na kukabidhiwa kadi namba 007194 huku
akitazamiwa katika ziara hiyo kuwa miongoni mwa viongozi waandamizi
watakaoshiriki mikutano ya hadhara itakayofanyika.






0 comments:
Post a Comment