Klabu ya Yanga ya Dar es salaam leo imethibitisha kuwa iko "Serious" katika michuano ya kimataifa msimu huu baada ya leo kuishushia kipigo "Kitakatifu" timu ya Platinum FC kutoka Zimbabwe cha jumla ya mabao 5-1.
Ushindi huo umepatikana katika dimba la Taifa Dar es salaam katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa kombe la Shirikisho barani Afrika.
Mabao ya Yanga yamefungwa
na Salum Telela 31, Haruna Niyonzima 43, Amis Tambwe 46 na Mrisho Ngasa
52, 89 huku moja la Platinum likifungwa na Kamusoko dakika ya 45
Ushindi huo ni mtaji kwa Yanga ambayo itarudiana na timu hiyo wiki mbili zijazo nchini Zimbabwe, kwani itahitaji sare aina yoyote ili isonge mbele.
Platinum FC italazimika kuifunga Yanga si chini ya magoli 4-0 ili isonge mbele.

0 comments:
Post a Comment