KWANINI EPL HAITAPOKONYWA NAFASI YA NNE (4) MSIMU HUU?
Kuna uvumi na fununu kwamba nafasi ya nne kwenye ligi kuu nchini
Uingereza inaweza kuondolewa kama hakuna timu yoyote itakayoingia robo
fainali kwenye michuano ya ligi ya mabingwa wa Ulaya kwa msimu huu ama
kama klabu ya Everton haitafika mbali kwenye michuano ya Europa.
Tukiachana na fununu na uvumi wa taarifa za kwamba EPL itanyang’anywa
nafasi ya nne hebu tuangalie taarifa sahihi kwenye swala hili ni zipi
kwa kujiuliza maswali machache ya muhimu:
Swali la 1: Nchi mbalimbali zimepewa nafasi ngapi?
Kwasasa msimamo unaonyesha nchi tatu za juu ambazo ni Hispania,
Uingereza na Ujerumani zimepewa nafasi nne (4) kila mmoja za ligi ya
mabingwa Ulaya wakati nchi tatu zinazofata yaani Italia, Ureno na
Ufaransa zimepewa nafasi tatu kila mmoja.
Ukiangalia orodha inaonyesha kuna timu ya kwanza mpaka ya mwisho yaani
1. Hispania, 2. Uingereza, 3. Ujerumani, 4.Italia, 5. Ureno na 6.
Ufaransa. Na msimamo huu unatokana na mgawo wa alama (coefficient) ambao
unatokana na pointi ambazo kila nchi inapata kutokana na jinsi klabu
zake zitakavyofanikiwa katika ligi ya mabingwa Ulaya na Europa.
Swali la 2: Mgawo wa alama (coefficient) unatafutwaje?
Mgawo unapatikana kwa kuangalia wastani wa alama ambao unapatikana kwa
KUGAWANYA ALAMA (points) ambazo klabu zinazoiwakilisha nchin fulani
inazipata katika michuano ya UEFA na EUROPA kwa IDADI YA KLABU hizo.
Halafu jibu litakalopatikana linajumlishwa na matokeo ya misimu minne
iliyopita kupata mgawo (coefficient).
Swali la 3: Alama zinapatikanaje?
Kila timu inapata alama mbili itakaposhinda na alama moja itakapotoka
sare, ingawa alama huwa zinagawanywa kwa nusu kwa mechi za hatua ya
kuvuka (qualifying rounds) na mechi za mchangani (play-off rounds).
Vilabu ambavyo vinafika hatua ya 16 bora, robo fainali, nusu fainali ama
fainali kwa UEFA na EUROPA huzawadiwa alama moja ya ziada kwa kila
hatua.
Pia kuna nyongeza ya alama nne kwa kushiriki kwenye hatua ya makundi kwa
ligi ya mabingwa na alama nne kwa kuvuka hatua ya makundi.
Swali la 4: Uingereza kwenye msimu huu wamepata alama ngapi?
Chelsea imepata alama 20, Arsenal 19.5. Manchester City 15, Everton 12,
Liverpool 10, Tottenham 11 na Hull City 2.5 hii ikimaanisha mpaka sasa
Uingereza ina jumla ya alama 90, ukigawanya kwa idadi ya timu ambazo ni
saba, Uingereza inapata mgawo wa alama 12.857 kwenye msimu huu kwasasa.
Swali la 5: Tukiangalia kwa misimu mitano iliyopita Uingereza iko wapi
kwenye msimamo?
Kiujumla Uingereza ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 79.677 kwa misimu
mitano iliyopita, yaani 18.357 (2010/11) + 15.250 (2011/12) + 16.428
(2012/13) + 16.785 (2013/14) + this year's 12.857.
Huku Hispania ikishika nafasi ya kwanza ikiwa na alama 94.427 na
ujerumani ikishika nafasi ya tatu ikiwa na alama 77.415.
Swali la 6: Kuna nchi inaweza kuchukua nafasi ya Uingereza mwaka huu?
Kiuhalisia haiwezekani kwasababu wapinzani wakubwa kwa Uingereza ni
Italia ambao kiujumla wamepitwa alama 14 kwenye msimamo, hasa
ukizingatia kwamba kwenye msimu wa mwaka 2013/14 Italia ilipata alama
14.166 wakai Uingereza ilipata alama 16.785
Swali la 7: Hivyo ni kweli Italia wanahatarisha nafasi ya nne kwenye
ligi ya “Primia”?
Ndiyo, hasa ukizingatia kwamba mpaka sasa wana timu sita kweny msimu
huu, ambapo Juventus wako kwenye hatua ya 16 bora kwenye ligi ya
mabingwa Ulaya huku Torino, Roma, Fiorentina, Napoli na Inter Milan
zikishiriki ligi ya Europa.
Pamoja na Italia kuwa na timu nyingi kwenye ligi ya mabingwa Ulaya na
ligi ya Europa kwa msimu huu lakini bado ni vigumu kuipita Uingereza
kwenye mgawo wa alama.
Swali la 8: Je ni msimu gani ambao Uingereza inaweza kupoteza nafasi ya
nne kwenye ligi ya mabingwa Ulaya?
Msimu wa 2015/16 nafasi ya nne itakuwa salama na Uingereza haitaweza
kupokonywa, msimu wa 2016/17 inabidi vilabu viilinde nafasi hiyo
kwaajili ya msimu huo lakini kama vilabu vya italia vitaendelea kufanya
vyema kwenye ligi ya mabingwa na Europa basi msimu wa 2016/17 nafasi ya
nne itakuwa hatarini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)






0 comments:
Post a Comment