Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imeelezea wasiwasi wake kuwa kura ya maoni kwa Katiba inayopendekezwa huenda isifanyike mwezi ujaokutokana na kusuasua kwa uandikishwaji wapiga kura katika daftari la kudumu lawapigakura mkoani Njombe.Akizungumza na waandishi wa habari, janamjini Njombe, Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva, alisema kuwaupigaji wa kura hiyo huendausifanyike Aprili 30, mwaka huu na badala yake utasogezwa mbele kupisha kukamilisha kazi ya uandikishaji wananchi katika daftari la kudumu lawapigakura kwa kutumia mfumo wa kielekroniki (BVR).Wakati Mwenyekiti huyo akisema hivyo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema serikali imekwishaipatia Nec, asilimia 70 ya fedha zote za BVRzinazohitajika na kwamba kinachotakiwa sasa ni kuandikisha wapigakura, kazi ambayo itafanyika kwa ufanisi pindi vifaa vyote 8000 vitakapowasili.Jaji Lubuva alisema kuwa daftari hilo ni moja kati ya hatua za kufikia kura hiyo ya maoni ya Katiba mpya na kuwa kura haitafanyika kama uboreshajiwa daftari hilo halitakamilika nchi nzima.“Vitu hivi vinakwenda kwa kufuatana kikikamilika kimoja kinafuata kingine, hatutapiga kura ya maoni kama hautakamilika uboreshaji wa daftari lakudumu la wapigakura kwa mfumo wa BVR mkoani hapa,” alisema Jaji Lubuva.Mwenyekiti huyo alisema licha ya msimamo wa serikali kuwa kura ya maoni ifanyike Aprili 30, mwaka huu, lakini kwa mwenendo wa uandikishajiwapigakura italazimika kusogezwa mbele.“Ndugu waandishi mwendo wa daftari la kudumu na nyinyi mnauona, hivyo tutatoa siku ya kupigia kura ya maoni kulingana natutakavyoona mwelekeowa uandikishaji, lakini siwezi kusema sasa kuwa imeahirishwa mpaka lini,” alisisitiza.Alisema uandikishwaji wananchi mkoani Njombe utaendelea hadi Aprili 15, mwaka huu.Kauli hiyo ni tofauti na iliyotolewa na Nec wakati uandikishaji unaendelea kuwa mkoani humo, utakamilika Aprili 12, mwaka huu.Jaji Lubuva alisema BVR kits 7,750 zipo njiani na baada ya kuwasili zitatumika nchinzima na ratiba itawekwa wazi na kwambakwa mkoa wa Njombezinatumika 250.Pinda wakati akizindua uandikishwaji wa daftari la kudumu la mpigakura, Februari 23, mwaka huu, katika halmashauri ya Mji wa Makambako mkoaniNjombe, alisema vitambulisho vinavyoandikishwa vitatumika katika kupiga kura ya maoni ya katiba hiyo.Mara kwa mara Rais Jakaya Kikwete alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa kura ya maoni kwa Katiba inayopendekezwa itafanyika Aprili30, mwaka huu.Tangu kuanza uandikishaji wa majaribio katika majimbo matatu ya Kawe, Kilombero na Mlele, Desemba mwaka jana, na Februari 23, mwaka huu,mkoani Njombe, kumekuwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ya mashine kushindwa kufanya kazi kwa muda wote, kutosoma vidole vyenye ngozingumu na uchache wa vifaa.Baada ya uandikishaji wa majaribio, Nec ilitangaza kuanza na mikoa mitatu ya Mtwara, Njombe na Ruvuma, lakini hadi sasa uandikishaji unafanyikakwa Njombe pekee na hadi sasa haujakamilika.Jaji Lubuva amekuwa akiwaeleza waandishi wa habari kuwa BVR kits 7,750 zipo njiani na zitawasili wakati wowote kwa kuwa serikali imetoa asilimia50 ya fedha.Wadau wa uchaguzi ambao ni vyama 22 vya siasa, vilivyokutana na Nec Februari 12, mwaka huu, waliitaka kuweka wazi ratiba ya uandikishaji,mzabuni wa vifaa, kiasi cha fedha kinachotakiwa na wapiga kura wanaokadiriwa kuandikishwa kila kata.Licha ya maswali ya wadau hao, majibu yaNec yamekuwa ni kuwa wanaamini uandikishaji utamalizika kabla ya Aprili 30, mwaka huu, ili daftari hilolitumike katika kura hiyo na uchaguzi mkuu.Hali iko hivyo, huku zikiwa zimebaki siku 26, ukitoa siku za Jumapili na sikukuu , ambazo uandikishaji haufanyiki, kufika siku ya kura ya maoni kamailivyotangazwa na serikali.HALI ILIVYO NJOMBEMachi 22, mwaka huu, wakati uandikishaji ulipokamilika katika mji wa Njombe, baadhi ya wananchi hawakuandikishwa kutokana na nyongeza ya sikumoja kutotosheleza kutokana na uchache wa vifaa.Mkazi wa Njombe, Freddy Kifasi, ameomba kuongezwa kwa muda zaidi kwakuwa alifika kituoni siku ya mwisho lakini hakufanikiwa kutokana nautaratibu uliopo kumtaka kuandikisha jina siku ya Jumapili na kwenda kuandikishwa Jumatatu, utaratibu ambao alidai hakuufahamu.Msimamizi wa uchaguzi katika mji huo ambaye pia ni Mkurugenzi wa mji wa Njombe, Venance Msungu, alisema hakuna nyongeza ya muda nakuwataka wananchi kuwa na subra hadi nec itakapotangaza nyongeza ya muda.PINDA: SERIKALI IMEJIPANGAWaziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema serikali imejipanga kuhakikisha uboreshaji wa daftari la wapigakura kwa mfumo BVR, unafanikiwa hivyo kilakata itapelekewa seti mbili au tatu ya vifaahivyo.Akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana, alisema hadi mwezi ujao, uandikishaji utakuwa umeanza nchinzima.Hata hivyo, Pinda hakueleza ni lini vifaa hivyo vitawasili nchini kwa kuwa wanaosimamia jambo hilo ni Nec yenyewe.“Uandikishaji kule Njombe umekwenda vizuri na tumejifunza kwamba maeneo ya mijini BVR ziwe nyingi tofauti na vijijini kwasababu preshahaikuwa kubwa vijijini kama mjini. Kwa sasa tunaona kila Kata tukiandikisha kwa siku saba na tukawa tumepeleka BVR mbiliau tatu,zoezi litakwenda vizuri,” alisema.Kuhusu kamati za kampeni kuhusu Katiba inayopendekezwa ambazo zinapaswa kuanza kazi Aprili Mosi, Pinda alisema jambo hilo linashughulikiwa naNec, lakini serikali imejipanga kuhakikisha kura ya maoni inafanyika Aprili 30, kama ilivyopangwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment