Akizungumza na Times Fm, Katibu Mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii, Dkt Donald Mbando amesema kiwango hicho kimepungua kutokana na uanzishwaji wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya ukimwi mapema kwa watu wanaoishi na maambukuzi ya virusi hivyo
Bado elimu ya unyanyapaa kwa jamii haijafanikiwa kwa kiwango stahiki kutokana na mienendo ya kuwatenga watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na kutopatiwa msaada na jamii inayowazunguka hali inayowafanya wajihisi wanyonge ndani ya jamii.
Maadhimisho ya Siku ya ukimwi Duniani kitaifa mwaka huu yanafanyika Mkoani Njombe
Kauli mbiu ya siku ya ukimwi duniani mwaka huu ni “Tanzania bila maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi,Vifo vitokanavyo na Ukimwi na Ubaguzi pamoja na unyanyapaa, Inawezekana.”






0 comments:
Post a Comment