Matokeo ya jana na ratiba Capital One Cup

Author
Manchester City ikicheza nyumbani ilijikuta ikiwaduwaza mashabiki wake baada ya kukubali kichapo cha mabao 2 bila majibu kutoka kwa Newcastle utd na kutupwa nje kabisa ya mashindano hayo. Nayo Tottenham hotspurs iliutumia vema uwanja wake wa nyumbani kwa kuichabanga vilivyo kabisa Brighton kwa jumla ya mabao 2-0. Nayo Southampton ikairarua Stoke City kwa jumla ya mabao 3-2. Kwa matokeo haya ya sasa, katika robo fainali ratiba itakuwa hiv Chelsea ?-? Derby Tottenham ?-? Newcastle utd Liverpool ?-? Bournemouth Southampton ?-? Sheffield utd

0 comments:

Post a Comment