Hotuba ya aliyekua kiongozi wa Libya Kanali Mu'uammar Qaddafi. Aliiandika siku chache kabla ya kifo chake.
--QADAFFI ANAANZA HIVI:
"Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah), Mungu mpaji, na mwenye rehema....
Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni
kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na
shule. Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi
kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo.
Nilisimama imara dhidi ya
Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani), alipomuua binti yangu
niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua mimi
lakini akamuua yule binti
yatima masikini. Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia
AU.
Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana
halisi ya demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka.
Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika. Alihitaji zaidi.
Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia
Marekani kuwa wanataka "demokrasia" na "uhuru". Hawakujua kuwa
"demokrasia" waliyoitaka ilikua ni mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye
nguvu zaidi huwala mbwa wadogo.
Walikua hawasikii wala hawaoni.
Walitaka "demokrasia". Wakasahau kuwa hata Marekani hakukuwa na huduma
za afya za bure, dawa bure, elimu bure na chakula cha bure. (Huduma hizi
za bure zilipatikana Libya tu).
Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure. Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.
Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado hawakuridhika. Lakini wapo
waliojua mimi ni mtoto wa Gamal Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na
kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen.
Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake nami nilikua
naipigania Libya kwa watu wangu. Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili
kuwaweka watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia.
Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika
historia. Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka
kuniua.
Ili achukue uhuru wetu, achukue haki yetu ya huduma za bure
za afya, huduma za bure za elimu, na chakula chetu; na kutuletea mfumo
mpya wa kimarekani wa kuiba uitwao "Ubepari"
Lakini wote katika
dunia ya tatu tunajua maana yake. Maana yake ni kuwa "washirika"
wanatawala mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia kuteseka.
Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu. Lazima niwe na msimamo. Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake.
Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula
bora, na huduma bora za afya. Mapenzi ya Allah yaliyowezesha
tukawasaidia kaka na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na shida.
Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu wangu, na wengine ambao ni kama wanangu; acha nife.!
Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga
uvamizi wa NATO. Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za
magharibi na nia mbaya za kikoloni. Na hapa nimesimama na ndugu zangu
waafrika, kaka na dada zangu waislamu kama ngao yangu ya matumaini.
Wakati wengine walipokuwa wanajenga majumba ya kifahari, mimi niliishi
kwenye nyumba ya kawaida na kwenye mahema. Siwezi kusahau maisha yangu
ya utoto kule Sirte.
Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu.
Na kama alivyokua Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika uislamu,
nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu, na sehemu kubwa niliwapa
wananchi.
Watu wa magharibi wameniita "kichaa", "mwendawazimu"
lakini wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu; ila waache
waendelee kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye himaya
ya kikoloni. Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa
watu wangu.
Nitapambana hadi pumzi yangu ya mwisho ili watu wangu wawe huru. Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki waaminifu na tuwe huru.
-- Mu'uammar Qaddafi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment