MIMBA YA JINI -08

Author

Hadithi ya kusisimua  #Mimba_ya_Jini -8-

Mtunzi: #Mzizi_Mkavu

SASA SIKIA FANYA HIVI #LIKE PAGE HII USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA USIWEMCHOYO KUSHARE KWENYE #MAGROUP #MARAFIKI NASUBIRIA SHARE ZIFIKE 250 NIPOST NYINGNE NOW

#LIKE #COMMENT #SHARE

ILIPOISHIA:
Alijiuliza kama akikitumia nini kitakuwa, alimtuma mtoto duka la dawa baridi akamletee kipimo kile. Baada ya kuletewa alikwenda msalani na kujisaidia haja ndogo na kuiweka kwenye kikopo kisafi na kurudi nacho chumbani.
SASA ENDELEA...
Alikiweka kile kikopo chini na kukichukua kipimo, alikifungua ili akitie kwenye kikopo chenye haja ndogo. Mara simu yake iliita alipoitazama ilikuwa inatoka kwa Shehna.
Aliipuuza na kukiweka kile kipimo kwenye haja ndogo ili kuhakikisha kama ana mimba kweli. Kilipogusa tu kwenye haja ndogo, alihisi kama tumbo limechafuka ghafla. Ajabu nyingine haja ndogo iliyokuwemo kwenye kikopo iligeuka damu mbichi iliyotoa harufu kali. Alishtuka akiwa anashangaa hali ile, alizidi kushtuka kusikia hali ya majimaji ukimtoka chini kama ya kuziona siku zake. Alipoangalia alishtuka kuona nguo yote umetota kwa damu. Chini damu ilitengeneza michirizi aliyotapakaa sehemu kubwa kuonesha ametokwa na damu nyingi.
Kizunguzungu kilikuwa kikali alijitahidi kunyanyuka kwa kujilazimisha na kufanikiwa kuishika simu yake. Aliitafuta namba ya mume wake kwa shida na kupiga na kupokelewa upande wa pili.
"Haloo," Mustafa alipokea.
"Mu..mu..me wangu na..na ..ku..fa," baada ya kusema vile simu ilimponyoka na yeye akajitupa chini kama mzigo na kupoteza fahamu.
Mustafa alishtuka na kujiuliza mke wake amepatwa na nini tena. Hakutaka kutoka kama jana yake kwa kumshtua sekretari wake, alimuaga kwa sauti ya kawaida iliyoficha siri nzito ndani.
"Sara nafika nyumbani mara moja."
"Mbona hivyo kuna usalama?"
"Kawada tu."
Alitoka hadi kwenye gari lake na kuwasha kuwahi nyumbani huku akijiuliza mkewe amepatwa na nini. Aliendesha gari kwa mwendo wa kasi hadi nyumbani, baada ya kusimamisha gari alikimbilia ndani.
Alipoingia ndani alishtuka kukuta damu imetapakaa chumba kizima. Alishtuka kuona kikopo kikiwa na damu na ndani yake kuna kipomo cha mimba.
"Mungu wangu mke wangu kafanya nini?" Mustafa alishika mikono kichwani.
Alimshika mkewe aliyekuwa amelala sakafuni ambaye alionekana kapoteza fahamu huku akiwa ametokwa damu nyingi. Alijikuta akishindwa afanye nini baada ya kujua mkewe kafanya kosa kwenda kinyume na maelekezo ya Shehna.
Alimnyanyua na kumpeleka bafuni ambako alimfanyia usafi na kumrudisha kitandani, lakini wakati huo bado alikuwa amepoteza fahamu. Alibaki njia panda asijue ampeleke hospitali au afanye nini. Akiwa katika taharuki simu yake iliita, alipoangalia ilikuwa inatoka kwa Shehna, aliipokea haraka.
"Haloo Shehna."
"Haloo Mustafa, vipi mbona kama una tatizo?"
"Ndiyo, mke wangu ana matatizo."
"Matatizo gani tena?"
"Yaani hata sijui, anatokwa damu."
"Kwanza upo wapi?"
"Nipo nyumbani."
"Ha! Umeondoka sangapi wakati nimeingia nimeliona gari lako."
"Sasa hivi."
"Basi mi nipo ofisini kwako, utawahi kurudi?"
"Shehna, yaani matatizo ya mke wangu unayaona madogo?"
"Siyo madogo ya kujitakia."
"Sasa unanishauri nini?"
"Kuhusu nini?"
"Tatizo la mke wangu."
"Ulikuwa unahitaji msaada wangu ipi?"
"Wa ushauri wako."
"Mpeleke hospitali."
"Si ulitukataza?"
"Lakini mkafanya."
"Siyo mimi ni mke wangu."
"Basi mpeleke hospitali kwa hilo sina msaada wowote kwako lipo nje ya uwezo wangu."
"Haina tatizo kwenda hospitali?"
"Mustafa mi siyo mganga, wahi hospitali utampoteza mkeo," Shehna alisema kwa sauti kali kidogo.
"Sawa nimekuelewa."
"Sasa unarudi saa ngapi?"
"Sijajua."
"Ukimpeleka hospitali lazima atapata kitanda, nitakusubiri ukichelewa nitaondoka."
"Sawa."
Baada ya kukata simu Mustafa alimchukua mkewe na kumuwahisha hospitali. Alipofika alipokelewa na wauguzi na kukimbizwa wadini na kumuacha Mustafa nje akisuburi.
Baada ya vipimo majibu yalionesha ujauzito umetoka. Mganga alimwita ofisini na kumweleza tatizo la mkewe.
"Vipimo vinaonesha ujauzito umetoka."
"He! Kweli alikuwa na mimba?" Mustafa alishtuka.
"Ndiyo kwani ulikuwa hujui?"
"Ha..ha....ndiyo."
"Vipi Bwana Mustafa mbona unababaika?"
"Kulikuwa na dalili lakini hatukuwa na uhakika."
"Aah! Bwana Mustafa, unaniangusha siku hizi suala la ujauzito si la kusumbuka kwa vile mkiwa na wasiwasi mnakwenda duka la dawa baridi ambalo nina imani siku hizi lipo kila kona, unanunua kipimo na kupata uhakika."
"Na..na sababu ya kutoka ujauzito?"
"Inawezekana alianguka na kulilalia tumbo."
"Duh! Sasa itakuaje?"
"Atafanyiwa usafi na kuongezwa damu kutokana na kupoteza damu nyingi kisha tutaangalia hali yake kwa kesho, ikiendelea vizuri tutamruhusu."
"Kwa hiyo naweza kumsubiri?"
"Hapana kaendelee na majukumu ya ujenzi wa taifa ila acha namba yako ya simu tutakujulisha hali ya mkeo, yangu utaangalia katika business card yangu," Daktari alimkabidhi kadi Mustafa.
"Nashukuru, lakini tatizo siyo kubwa?"
"Siyo kubwa, damu ndiyo iliyopotea nyingi, lakini jioni ya leo atakuwa vizuri."
"Nashukuru dokta."
Mustafa alitoka na kurudi nyumbani kufanya usafi wa damu iliyomtoka mkewe. Lakini alishtuka kukuta nyumba ipo katika hali ya usafi hakuna hata na chembe ya damu sehemu.

Itaendelea SHARE NIPOST NYINGNE NOW...  ....

0 comments:

Post a Comment