MIMBA YA JINI -07

Author

Hadithi ya Kusisimua  #Mimba_ya_Jini-7-

Mtunzi: #Mzizi_Mkavu

SASA SKIA ILI UPATE MWENDELEZO WA HADITHI HII YA KUSISIMUA #LIKE PAGE HII UWE WAKWANZA KUPATA MWENDELEZO WA HADITHI HII YA KUSISIMUA USIWE MCHOYO #LIKE PAGE #SHARE STORY KWENYE #MAGROUP #MARAFIKI NIPOST NYINGNE NASUBIRIA SHARE ZIFIKE 250 NIPOST NYINGNE.

ILIPOISHIA:
"Samahani shoga sikuwa na maana hiyo bali kukujua tu," Husna alijitetea.
"Si nimekueleza utanijua wasiwasi wako nini?"
"Kuhusu ujauzito siwezi kuamini japokuwa nina dalili zote za ujauzito huenda ni malaria, mi nataka kupima ili nihakikishe."
"Husna naomba suala lako usilichanganye na masuala ya Kizungu," Shehna alimpa onyo mke wa Mustafa.
SASA ENDELEA...

"Sawa nimekuelewa shoga."
"Najua majibu yako yamejaa unafiki sasa ukienda kinyume tusilaumiane."
"Nimekuelewa shoga."
"Nataka hili umweleze na mumeo, sawa?" Shehna alisema kwa sauti kali.
"Sawa."
Simu ilikatika na kumfanya Husna arudi kwenye kochi na kukaa, safari ya kwenda duka la dawa baridi ikakatika ghafla. Mustafa alishtuka na kumuuliza mkewe.
"Vipi mbona huendi dukani?"
"Shehna amekataa."
"Amekataa nini?"
"Nisiende kununua kipimo cha mimba wala nisikitumie."
"Amejuaje unataka kwenda kununua?"
"Nimemwambia nataka kuhakikisha kama kweli nina ujauzito nakwenda kununua kipimo cha mimba."
"We unasemaje?"
"Niseme nini? Mmh! Ipo kazi."
"Kwa hiyo huendi?"
"Amesema suala la ujauzito wangu tusichanganye na mambo ya Kizungu."
"Kwa hiyo hata ukiumwa?"
"Sijui muulize wewe."
"Mmh! Sawa."
Walikubaliana kutotumia dawa za Kizungu kipindi chote cha ujauzito japokuwa Husna moyoni hakuamini kama alikuwa mjamzito na kutaka kufanya kwa siri ili kupata uhakika.
***

USIWE MCHOYO #LIKE #SHARE UNIPESAPORT YA KUTUMA MWENDELEZO WAKE NASUBIRIA #SHARE ZIFIKE 250 NIPOST NYINGNE

Sara baada ya bosi wake kuondoka katika mazingira tata alifunga ofisi na kuchukua vitu vya bosi wake ampelekee nyumbani ikiwa pamoja na kwenda kujua nini kilimsibu.
Alikodi gari na kuelekea kwa bosi wake, akiwa njiani ghafla usingizi ulimpitia. Ajabu aliposhtuka alijikuta kitandani kwake akiwa amelala na mizigo ya bosi wake ameishikilia mkononi.
Alipopepesa macho alishangaa kuona jua kama la asubuhi. Alinyanyuka kitandani na kushangaa kukuta mlango ukiwa wazi.
Aliweka vitu kwenye kochi na kuangalia saa ya mkononi iliyomuonesha ni saa mbili asubuhi. Alishangaa kujiona akiwa nyumbani amelala na vitu alivyokuwa akimpelekea bosi wake.
Alijawa na mawazo na kujiuliza alipotoka kazini na kukodi gari alimwambia dereva ampeleke kwa bosi wake au nyumbani kwake? Akakumbuka alimwambia ampeleke kwa bosi na si nyumbani.
Alijiuliza kama alikwenda nyumbani kipi kilimsibu mpaka akalala na nguo zake bila kuvua viatu na mkoba wenye ‘laptop' na koti la bosi wake. Bado alikuwa njia panda kuhusiana na kurudi nyumbani na kulala bila kula wala kufunga mlango.
Mara simu iliita ilikuwa ya bosi wake, aliipokea.
"Haloo bosi."
"Sara upo wapi?"
"Nyumbani."
"Unaumwa?"
"Hata siumwi."
"Mbona hujafika kazini?"
"Bosi hata sijui niseme nini?"
"Basi wahi ofisini huwezi kuamini nina nusu saa nipo nje ofisi imefungwa."
"Mungu wangu, jana nilijisahau na kuondoka na funguo."
"Basi wahi."
Sara alioga haraka na kubadili nguo kisha alikodi bodaboda kuwahi kazini huku akimuhimiza dereva akimbize pikipiki.
Alifika ofisini baada ya dakika tano, Sara alimsalimia bosi wake na kufungua ofisi, Mustafa akaingia ndani.
Alimkabidhi vitu vyake na kurudi kwenye eneo lake la kazi kumalizia kiporo ndipo amuuliza bosi wake jana ilikuwaje na kumweleza yaliyomtokea.
***
Husna mke wa Mustafa akiwa nyumbani peke yake moyo ulimsukasuka juu ya hali aliyonayo ambayo alielezwa ni ujauzito lakini alikatazwa kutumia kipimo cha Kizungu kutambua kama ni mimba.
Alijiuliza kama akikitumia nini kitakuwa, alimtuma mtoto dawa katika duka la dawa baridi akamletee kipimo kile. Baada ya kuletewa alikwenda msalani na kujisaidia haja ndogo na kuiweka kwenye kikopo kisafi na kurudi nacho chumbani.

Itaendelea SHARE KWA MARAFIKI MAGROU NIPOST NYINGINE NOW....

0 comments:

Post a Comment