Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu nilichoweza.
Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna ng’ombe, niliiba
maziwa kila siku na kumpelekea kwao.
Akanenepa!! Penzi letu likawa huru alipo anza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi. Alinifundisha.
Nikaegemeza maisha yangu yote kwake.Akanifanya nikawa mtumwa
wa ngono kila nikienda chumbani kwake.
Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa ndiye mume
wangu mtarajiwa, kwa nini nikatae?
Nilimkubalia kila kitu.Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku
zangu. Kweli nilikuwa.msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo
lakini sikutaka kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu.
Nilipenda tututmie kinga lakini aliipinga sana. Nikapata mimba ya
kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa
nyumbani nikafanyaalivyotaka. Kwa mara ya kwanza nikatoa mimba. Haikuniuma sana!!
Niliamini kuwa ni yeye atakuja kunioa na.atanifichia aibu hii.
Nilitegemea sasa tutaanza kutumia kinga.
Lakini hapana haikuwa hivyo. Aliendelea kunilaghai. Tayari aliujua
udhaifu wangu. Alinishika hapa na pale. Nikishtuka tayari amefanya
anavyojua.
Pombe kidogo na nyingine kidogo. Nikazoea lakini
nikawa nawahi kulewa. Akautumia udhaifu huu kunifanyia jambo baya
lililonifanya
niandike haya kwako. Akaniingilia kinyume na maumbile. Alinilawiti!!
Nilishindwa kumshtaki popote.
Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa. Mume
asiyejulikana hata kwa wazazi.
Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu mbadala. Najuta
kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu.
Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona katika kioo ukatoweka, simu za mara
kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali sana kwangu. Hakutaka niende kwake.
Wakati huo nilikuwa nasoma chuo. Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na
tunakuwa marafiki tena. Anasema ananipenda na atanioa. Ananilewesha na
kunitumia kinyume na maumbile.
Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha
nabakimwenyewe katika msoto. Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema
nini mimi?
Ninajua alishindwa kusema neno
moja tu. Tuachane!! Nilijua tayari ameniacha!!!
Afya yangu ikadolola sana, nikalazimikakwenda kupima hospitali. Sikuwa
na virusi. Nikapewa ushauri nikautumia. Siku zikasonga nikampata
mwanaume mwingine. Huyu alikuwa ananijali
sana.
Nikaanza kumsahau yule aliyenitenda..Nilipomaliza chuo akajitambulisha nyumbani na
alitaka kunioa. Akanioa kweli.
Maisha yakaanza. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa
tatu. Sikuwa nabeba mimba. Mume wangu alikuwa mvumilivu sana, hakuwa hi kunilaumu.
Lakini niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali. Nikaambiwa
kizazi change kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia mapenzi
ya kinyume na maumbile yamenivuruga kabisa.
Nililia sana huku nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu kwangu. Dunia haikuwa mahali
pangu sahihi.
Nimekuandikia barua hii mdogo wangu.Uisome mwenyewe!! Lakini uwasimulie wengi baada ya
kifo changu. Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyika na kufanya mambo magumu kuwaridhisha
wapenzi wao.
Waambie watakufa kwa mateso
kama mimi. Wasipokusikiliz a usijisikie vibaya maana hata mimi nilikuwa siwasikilizi watu
waliponambia lolote kuhusu yule
mumemdanganyifu. Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!!
Nimekuandikia wewe kwa kuwa u mwandishi.
Japo kwa sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi siku moja ya kuwafikishia wasichana
hawa.
Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume mwenzako AMENITENDA HIVI!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment