Mahakama yazuia baadhi ya Ibara za sheria

Author
Mmoja kati ya waandamanaji dhidi ya sheria mpya ya kupambana na ugaidi akamatwa na polisi mjini Nairobi tarehe 18 Desemba mwaka 2014.Nchini Kenya, Mahakama imezuia Ibara muhimu za sheria dhidi ya ugaidi ambayo iliibua mvutano kati ya wanasiasa tangu mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2014.



Serikali ya Kenya imekua ikiitetea sheria hiyo, ambayo kwa mujibu wake ni muhimu kwa kujilinda kutokana na tishio la kundi la Al-Shebab.
Lakini adhabu zilizopendekezwa katika sheria hiyo zilichukuliwa kiubabe na upinzani pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu. Adhabu hizo zinachukuliwa kuwa zinakiuka haki msingi za binadamu.
Jaji wa Mahakama kuu amezuia Ibara 8 za sheria hiyo, "kwa sababu, amesema, zinakiuka haki za binadamu."
Miongoni mwa vifungu hivyo vya sheria vilivyozuiliwa ni ile ambayo inatoa adhabu ya miaka mitatu jela na faini ya dola 55,000, kwa uchapishaji bila ruhusa wa makala au kutafuta habari " ambazo zitatatiza uchunguzi au operesheni ya kupambana dhidi ya ugaidi ".
Ibara nyingine iliyozuiliwa ni ile ambayo imekua imeipa uwezo polisi kufanya udukuzi wa maongezi ya simu. Na ya tatu ni ile iliyokua inatoa idadi ya wakimbizi 150,000 kutoka Somalia ambao wanatakiwa kupewa hifadhi nchini Kenya, wakati wakimbizi wa Somalia nchini Kenya wakati huu ni 600,000.
Upinzani ndio uliowasilisha Mahakamani barua ya kupinga sheria hiyo. Kwa wiki kadhaa, upinzani na wanaharakati wa haki za binadamu wamekua wakilani sheria hiyo kwamba inakiuka haki za binadamu, na hivyo " nchi kuwekwa chini ya mamlaka ya polisi."
Kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, amekaribishwa uamuzi wa Mahakama ambapo amesema " uamzi wa Mahakama unaipa sifa kubwa Kenya."
Bungeni, sheria sheria hiyo ilizua mijadala mikali, lakini hatimaye ilipitishwa tarehe 18 Desemba. Uamuzi wa Mahakama Kuu ni pigo kubwa kwa rais Uhuru Kenyatta, ambaye alitetea kwasheria hiyo, akielezea kuwa inawalinda raia.
Muswada wa sheria kuhusu usalama uliwasilishwa Bungeni baada ya mfululizo mpya wa mashambulizi yaliyotekelezwa na kundi la Al-Shebab mwishoni mwa mwezi Novemba na mwanzoni mwa mwezi Desemba, kaskazini mashariki mwa Kenya, katika mkoa wa Mandera. Mashambulizi ambyo yalisababisha yaligharimu maisha ya watu wengi.

0 comments:

Post a Comment