Hatimaye klabu ya Simba imetwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Mapinduzi mwaka 2015 kwa kuifunga Mtibwa Sugar kwa penati 4-3 baada ya kushindwa kufungana katika muda wa kawaida wa Dakika 90.
Simba ambayo ilianza michuano hii kwa kusuasua baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza, imekabidhiwa kombe ambalo ni jipya na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein pamoja na kitita cha shilingi Milion 10 pale pale katika uwanja huo wa Amani Zanzibar.
Waliofunga penati za Simba ni Awadh Juma, Ramadhani Kessy, Hassan
Isihaka na danny Sserunkuma huku penati ya Shaaban Kisiga ikiokolewa na
Golikipa wa Mtibwa Said Mohamed.
Kwa upande wa Mtibwa, waliofunga penati ni Ali Lundenga, Shaaban Nditi na Ramadhan Kichuya wakati penati ya Ibrahim Rajabu 'Jeba' ikigonga mwamba na penati ya mkongwe Vincent Barnabas ikiokolewa na golikipa wa Simba Ivo Mapunda.
Katika mchezo huu Golikipa Ivo Mapunda aliingia katika dakika ya 90 kuchukua nafasi ya Golikipa Manyika Peter.
Mchezaji bora wa michuano hii ni Salim Mbonde wa Mtibwa Sugar na Mfungaji bora ni Simon Msuva wa Yanga na Golikipa bora wa michuano hii ni Said Mohamed wa Mtibwa Sugar.

0 comments:
Post a Comment