PRISCA -18

Author
PRISCA
SEHEMU YA KUMI NA NNE

ILIPOISHIA

Prisca na Rose walikuja na kuninyanyua pale chini kisha tukaanza kutoka nje kwa kunyata, tulipochungulia kwa nje tulikuta kundi kubwa la majambazi waliokuwa wameshika bunduki zao imara kabisa kwa kupiga kwa mtu yoyote, walikuwa wamekaa serious huku wakitangaza kwa kutumia kipaza sauti

“hatuna shida na nyie sisi tunataka disk yetu pamoja na flash yetu”walitangaza

SONGA NAYO

Nilianza kujihisi kufakufa kwani hakukuwa na mlango mwingine wa kutorokea kwani zaidi ya ule ambao majambazi walikuwepo pale, moyoni bado nilikuwa na uchungu kumuona mama yangu mzazi akiwa chini kanyamaza kimya, uchungu wa kulipa kisasi ulianza kunipanda kwani nilikuwa nampenda sana mama yangu japo sikuwa na uhakika kama kweli amekufa

Wale jamaa walianza kuhesabu huku wakiweka silaha zao vizuri kwaajili ya mashambulizi, Prisca na Rose nao walianza mipango ya kutoka pale kwa nguvu huku wakishambulia kininja

“moja, mbili, taaa”

Kabla hawajamaliza kuhesabu nilishangaa kusikia milio ya risasi ikilindima huko nje huku nikisikia sauti za vilio na watu wakidondoka kama mizigo, mara nikaanza kusikia ving’ora vya Police vikija kwa kasi ya ajabu pale kwenye eneo la tukio, majambazi nao walianza kushambuliana na Police huku kila mmoja akitaka kushinda vita ile

Hapo na sisi tulipata upenyo wa kutoka nje kwa speed ya ajabu huku tukipiga wale majambazi, tulifanikiwa kuingia mpaka kwenye gari moja lililokuwa mbali kidogo na pale tulipokuwepo, kasheshe ilikuwa ni kuipata funguo ya gari kwani inaonekana mwenye gari alishakimbia baada ya kusikia ule mtiti uliokuwa unaendelea pale nje, kwakuwa mimi nilikuwa mtalamu wa magari nikakata nyaya mbili kwa ufundi mkubwa kisha nikiziunga tena

Lile gari liliwaka na kurudisha reverse kidogo kisha nikatoka kwa mwendo wa kasi sana, upande tuliokuwa tunaelekea ni ule upande wa majambazi waliokuwa wanapigana na maaskari kwahiyo yalikuwa yamezubaa, nilipita pale na kupiga break kisha nikashuka kwa tahadhari na kuingia ndani ya nyumba yetu ili kumchukua mama yangu kwani alikuwa kwenye hali mbaya sana

Nilifanikiwa kumchukua mama yangu na kuanza kutoka nje ili nikampakie kwenye gari niweze kumpeleka hospitali nione kama ataweza kupata nafuu kwani kwa muda huo mapigo yake ya moyo yalikuwa yanaenda taratibu sana

“Prisca endesha gari mimi nipo nyuma na mama yangu” nilimwambia Prisca

"Sawa David" alisema na kuanza kutimua mbio

Tulitoka pale kwa speed mpaka wale majambazi yaliruka pembeni kwani yalishangaa ule mwendo tuliopita nao

“wanatoroka fuata fuata” alisema jambazi mmoja baada ya kutuona

Majambazi yaliwasha magari yao na kuanza kukimbizana na sisi, wale maaskari nao waliingia kwenye magari yao na kuanza kufukuza yale majambazi. Barabara ilichafuka sana kwani risasi zilikuwa zinaridimwa ili kushambuliana. Tulifika barabara ya Kilwa na kuanza kushuka upande wa kuelekea Mbagala nia na madhumuni ni kumpeleka mama yangu hospitali ya Temeke.

“Prisca ongeza mwendo tafadhali” nilisema

Prisca alizidisha mwendo lakini alikuwa anapita barabara ya pembeni kwani njia kuu kulikuwa na foleni kubwa sana, tulifika sehemu tulishidwa kupita kwani watu waliokuwa na magari walikuwa mengi sana

“David muwahishe mama hospitali sisi acha tupambane na hawa majambazi” alisema Rose

“sawa ngoja mimi niwahi” nilisema

“fanya haraka” alisema Prisca

Nilishuka huku nikiwa nimemuweka mama yangu begani kisha nikaanza kutimua mbio, japo mama alikuwa mzito lakini nilijitahidi kujikaza kwani nikifanya uzembe kidogo naweza nikamkosa mama yangu, watu walikuwa wananishangaa kwa kitendo nilichokuwa nakifanya kwani kilikuwa kitendo cha kijasiri sana,ggafla nilianza kusikia milio ya risasi ikianza tena, watu walianza kutelemka kwenye magari yao kama vichaa na kuanza kutimua mbio za hatari

Bahati ilikuwa upande wangu kwani wakati nakimbia niliona mtu akiendesha bajaji, nilisimama mbele yake na kumpakia mama yangu kwenye ile bajaji yake

“Please naomba tuwahi hospitali ya Temeke mara moja” nilisema

“sawa” alisema huku akitimua ile bajaji

Tulifanikiwa kufika hospitali na wasaidizi wa hospitali walikuja na kumchukua mama yangu huku mimi nikifuata wanapoelekea, walimuingiza wodi ya wagonjwa mahututi kisha wakaanza kumuhudumia, walikuja na kunitoa nje ili waendelee kumuhudumia mama yangu

“kijana usijali mama yako atapona tu” daktari alisema

“naomba ufanye ivyo daktari” nilisema

Kichwani bado nilikuwa nawaza ile vita iliyokuwa inaendelea kule nili[powaacha wakina Prisca na wale majambazi, kwakuwa mama yangu alishafika kwenye mikono salama nikaona bora niende kuwasaidia wakina Prisca katika ile vita, nilitoka pale hostpitali na kuanza kutimua mbio kuelekea pale nilipoacha ile vita ikiendelea

Nilifika pale na kukuta hali ikiwa kimya sana kwani hakukuwa na mtu hata mmoja eneo lile, nilianza kutembea kwa tahadhali kubwa sana nisije nikaingia kwenye matatizo kwani hali ilikuwa ya kutisha sana, nilipita mpaka kwenye gari moja na kujificha sababu nilisikia watu wakiongea, zile sauti zilikuwa zinakuja mpaka upande niliokuwepo

“Yule pale” alisema jamaa mmoja na kunyoosha bunduki yake ili kunipiga

Ila kabla hajanipiga risasi nilishangaa wote wawili wakidondoka chini kama mizigo, nilibaki nikishangaa kwanini wale jamaa walidondoka chini, nilipoangalia macho yangu pembeni niliwaona Prisca na Rose wakitokea huku wakitabasamu kuniona

“David kama unaweza peleka hii disk kituo cha Police haraka iwezekanavyo kwani hali ni mbaya sana” Prisca alisema huku akinipatia ile flash iliyokuwa na siri za wale jamaa

“sawa ila si tunaenda wote?” niliuliza

“ndiyo ila wewe ndiyo utakayeingia” alisema

Tulianza safari ya kuelekea kituo cha police kilichopo Chang'ombe usalama, tulifika pale na mimi nikaenda kuingia pale kituoni ili nikaeleze kila kitu kilichiotokea na ni siri gani zilizokuwepo kwenye ile flash, nilikaribishwa na kukutana na afande mmoja kisha nikaanza kumuelezea kila kitu kilichotokea na kumpatia ile flash niliyoenda nayo.
Yule afande alikuwa ananiangalia kwa umakini mkubwa sana huku akiandika vitu kwenye daftari

Nilitoa maelezo yote huku nikiwa sina imani na Yule askari kwani sura yake ilikuwa inaonekana alikuwa mpenda rushwa sana, nilipomaliza na kukabidhi kila kitu nilitoka nje na kuungana na wakina Prisca ili tuondoke, safari hii ilikuwa ni kuelekea nyumbani kwetu Keko Machungwa ili tukapange mipango ya kufanya ya kuwakwepa wale jamaa, tulifika mpaka nyumbani kwangu Keko Machungwa na kuingia moja kwa moja mpaka ndani na wakina Prisca

Niliingia nyumbani kwangu bila hata watu kujua kwani ilikuwa ni jioni na watu hawakuwepo pale nje, niliamua kutoka ili nikakutane na watu angalau wawili watatu niweze kuwauliza nini kinaendelea pale mtaani, nilitoka nje na kuanza kuongea na baadhi ya watu nijue kama walikuja watu wowote pale mtaani, watu walinishangaa kuniona bado nipo hai kwani wengine walishajua kwamba nimekufa

Nilipiga story mbili tatu na kuamua kurudi chumbani kwangu ili nikaongee na wakina Prisca, wakati nafika pale nilishangaa kuona gari likitoka kwa speed ya ajabu sana, kwanza nilitahamaki kuona ile gari likitokea maeneo ya nyumbani kwangu, akili ilianza kunicheza kwamba kutakuwa na tatizo limetokea

Nilipofika chumbani kwangu nilishangaa kuona wakina Prisca hawapo, niliendelea kuangalia mule ndani mara nikashangaa mtu akija nyuma yangu na kurusha teke, kwakuwa nilikuwa nimemuona kwenye kioo cha chumbani niliinama na kupiga teke la nguvu lililompeleka yule jamaa chini, nilimfuata na kumpiga kabari ya nguvu

“naomba uniambie wale wanawake wameenda wapi?” nilimuuliza

“nitakuambia mkuu” alisema

“aya niambie” nilisema

“wamechukuliwa na kundi letu na sasa wanapelekwa kwenye msitu wa Mabwepande ili wakauwawe” Yule jamaa alisema

Nilishangaa wamewezaje kuwateka wale wanawake wakati walikuwa hatari sana

“mmewezaje kuwateka?” nilimuuliza

“kuna dawa tuliwapulizia chumbani mwako” alisema

Nilimchukua yule jamaa na mimi tukatoka nje na kuichukua ile gari niliyokuja nayo, lengo langu kubwa ilikuwa ni kuwaokoa wakina Prisca kwani walinisaidia sana kwenye matatizo yangu

“lazima niwaokoe” nilijisemea

ITAENDELEA…………

Je, David atafanikiwa kuwaokoa wakina Prisca?
Je, mama yake na David atapona?

posted from Bloggeroid

0 comments:

Post a Comment