Marafiki Club~11
By Sparner Boy 0765148781
Ilipoishia
Mariam alitoka kwenye kifua cha Roy,walipoangalia mlangoni walishtuka kumwona Husna na Roy alijua kilichokuwa kinafuata ni kifo..
Endelea..
Husna akiwa amesimama pale mlangoni,aliendelea kuwapigia makofi uku machozi yanamtoka kwa wingi na baada ya hapo alifunga mlango akatoka nje pasipo kuongea neno lolote.Baada ya Husna kuondoka Roy alimgeukia Mariam akamnasa kibao cha uso huku anamlaumu kwa matatizo aliyomsababishia.Mariam alilia akawa anamuomba Roy amuombee msamaha kwa Husna kwani yeye ni yatima na hana ndugu wala mzazi yoyote kwenye hii dunia Husna alimwokota mtaani na kumlea.Roy alimwangalia kwa hasira uku anavaa nguo zake kwani alishajua kuwa pale pameharibika na alikuwa anasali kimoyo moyo Mungu amsaidie aweze kutokea eneo lile akiwa salama.Alipojaribu kufungua mlango,aligundua kuwa Husna amewafungia ndani.Walichanganyikiwa kwani hawakujua Husna ana lengo gani juu yao.
Husna alitoka akalekea Stoo na kuchukua mpira pamoja na ndoo kisha akaenda kwenye gari na kuanza kunyonya mafuta huku hasira zikiwa zimemfika shingoni,ndoo ilipojaa alianza kunyunyiza chumbani kwa Mariam pamoja na sebuleni huku analia kwa kwikwi na kufanya rangi yake nzuri ya blown kubadilika na kuwa nyekundu kwa sababu ya Hasira na alipohakikisha nyumba nzima amenyunyiza petroli alipiga kiberiti nyumba ikaanza kuungua moto.
* * *
Roy na Mariam wakiwa chumbani huku hawajui kinachoendelea, mlango ulisumkumwa Husna akaingia na kuufunga kama mwanzo kisha akauegemea na bila kupoteza muda alitoa bahasha mbili akambabidhi Roy aliyepokea huku anatetemeka.Roy kabla hajauliza chochote Husna alimwambia:
"ile kazi inaanza jumanne,Hiyo bahasha ndogo utasoma kabla ya kazi lakini hiyo Bahasha kubwa utasoma baada ya kumaliza kazi kwa sasa hutaweza kuisoma"
Wakati wanaendelea kuongea walianza kusikika harufu ya petroli.Roy na Mariam hawakujua harufu ile ilipokuwa inatokea,harufu ile ilizidi kuwa kali lakini kabla Roy hajauliza ilipokuwa inatokea harufu ile,Husna alimwangalia Mariam na kumwambia
"Mariam nimekuwa kama dada pia mama yako leo unanifanyia hivi kweli?"
"nisamehe dada Husna ni shetani tu naomba msamaha wako"
wakati Husna na Mariam wanabishana,moshi ulianza kuingia mle chumbani kupitia chini ya mlango wote wakaanza kukohoa na mpaka wakati huo Roy na Mariam hawakujua moshi ule unapotokea,Roy aliinuka pale kitandani akamsukuma Husna pembeni akafungua mlango na kutoka nje.Alipofika sebuleni hakuamini kwani sebule yote pamoja na chumba cha mariam zilikuwa zinateketea kwa moto uliokuwa umesambaa nyumba nzima isipokuwa kile chumba walichokuwepo,Alirudi haraka chumbani na lengo lake awape Husna na mariam taarifa kuwa nyumba inaungua moto.Ile anaingia chumbani alipishana na Mariam anatoka nje akikimbia huku analalamika kuwa Husna anataka kumuuwa.Roy alishtuka na alipoingia chumbani alishangaa kumuona Husna anateketea kwa moto huku analia kwa uchungu.Roy alijaribu kumsogelea lakini akagundua kuwa kwa mda mfupi tayari Husna alikuwa ameungua Vibaya,Alijiuliza ule moto umefika saa ngapi mle chumbani lakini hakuwa na jibu.Wakati anawaza hayo alisikia Mariam akimwita kwa nje
"Roy njoo achana nae alitaka kuniua utakufa uko ndani mpenzi wangu"
Roy aliondoka haraka uku machozi yakimtoka kwani kitendo cha kumpoteza Husna kilimuumiza sana na hakujua nini hatma ya maisha yake kwa wakati ule.alitoka na kuacha nyumba ikiteketea kwa moto.Roy alipotoka nje na kumuona Mariam kitu cha kwanza alimwambia amueleze ilivyoluwa mpaka Husna akateketea kwa moto ndani ya muda mfupi kiasi kile,Mariam alimwambia kuwa Husna alijaribu kumnyonga yeye akamng'ata na kufanikiwa kukimbia ila vitu vingine hafahamu.
Baadhi ya majirani walikuja na kujaribu kuuzima moto ule ila walishachelewa kwani nyumba nzima iliteketea Husna akiwemo mle ndani na mpaka inafika saa 11 jioni nyumba ile ilikuwa imebaki kama gofu.
Roy na Mariam walilia sana ila haikusaidia kwani kama ni ajali imeshatokea
Giza lilianza kuingia,waliwaza sana watakapolala kwa usiku ule na mbaya zaidi Mariam hataweza kutoka nje ya geti kwani hakuwa na nguo yoyote zaidi ya Kanga moja aliyokimbia nayo kwenye mkasa ule,alijilaum kwa nini hakwenda na nguo zake chumbani kwa Roy asubuhi ile.Wakati wanawaza itakanyokuwa Mariam alimwambia Roy kuwa walale kwenye gari Roy alifurahia wazo lile na walipopanda kwenye gari Mariam akasema
"kaka Roy funguo zipo itatubidi tukatafute gest tulale gari tunalo tuanaweza kwenda popote"
"ok;ila sasa huna nguo itakuwaje"
Mariam alijiangalia na kunyamaza kimya kwani hakuwa na ujanja wa kutoka nje ya geti lile.Walipanda kwenye gari wakafunga vioo na kutulia kimya tayari kuutafuta usingizi.Baada ya muda mfupi Mariam alianza kukoroma Lakini kwa upande wa Roy usingizi ulimpaa kabisa mda wote alikuwa anamkumbuka Husna.Wakati yupo kwenye dimbwi la mawazo alikumbuka zile bahasha Husna alizomkabidhi na akamwambiea ile ndogo asome isipokuwa bahasha kubwa ambayo alitakiwa kuisoma baada ya kazi,haraka alianza kuifungua akiwa na shauku ya kujua kilichokuwa kimeandikwa ndani.
Itaendelea

posted from Bloggeroid
0 comments:
Post a Comment