MARAFIKI CLUB -07

Author
Marafiki Club~07

By Sparner Boy 0765148781

Ilipoishia..
Wakati anajiuliza swali lile kuna meseji iliingia kwenye simu yake na alipoisoma hakuamini alitamani ile iwe ndoto ila haikuwa hivyo
Endelea..
Meseji ile ilikuwa imetoka kwa boss wake na ilikuwa inasema
"Roy lazima wewe utakuwa ni mchawi sasa tutapambana mpaka mwisho tuone nani bingwa na nitakupata tu"
Roy alisoma ujumbe ule mara mbili mbili na baada ya kuona haelewi aliweka simu mfukoni akafungua mlango na kutoka sebuleni uku anaita jina la Husna.
"dada Husna hayupo ametoka"
Alijibu Mariam na kutoka jikoni alipokuwa anaanda chai,alikuwa ndani ya vazi la kulalia kitendo kilichompa wakati mgumu Roy,Roy alijaribu kuyakwepesha macho yake yasimuangalie mrembo yule mwenye rangi ya chocolate na umbo lenye kumtamanisha mwanaume yoyote.
"amekuaga?"
"hapana ila ni kawaida yake kutoka asubuhi sana na kurudi saa nne nne ivii"
"Ok naomba nifuate"
Aliongea Roy na kutangulia chumbani kwa Husna uku Mariam anamfuata.Walipofika chumbani Roy alifunga mlango kwa ndani uku Mariam bado amesimama pembeni ya kitanda anashangaa.
"kaka Roy kisa cha kufunga mlango nini?"
"nimefunga ila nataka utoke humu chumbani bila kufungua huo malango"
"haa,,siwezi kutoka"
"hakuna mlango mwingine wowote tofauti na huu"
"hapana"
Roy alimweleza Mariam kuwa asubuhi alipoamka hakumkuta Husna ila mlango wa chumbani ulikuwa umefungwa kwa ndani,Mariam alicheka sana akasema
"sasa amepitia wapi jamani utakuwa hujaangalia vizuri"
"Mariam nakuapia ni kweli sijui Husna alipopita,mpaka naogopa"
Roy alijitahidi kumsisitiza Mariam amuamini ila Mariam hakuonekana kujali alimfuata pale kitandani akamshika kichwa na kumuambia asiwe na mawazo kama hayo,alimpiga busu la kwenye shavu,taratibu akaanza kupiga hatua kuelekea sebuleni.
Roy alikaa mle chumbani akiwa na mawazo ya meseji bos wake aliyomtumia,Wakati yupo kwenye dimbwi la mawazo mlango ulisukumwa na Husna akaingia na moja kwa moja akamfuata Roy pale kitandani na kumpiga busu la nguvu mdomoni ila Roy alimwangalia tu Husna na kuendelea kushika tama kwa huzuni.
"mpenzi tatizo nini unashika tama"
"Husna nina wasiwasi na wewe ivi umepita wapi asubuhi,na kule hotel pia ilikuwa kama leo,nina wasiwasi kuwa wewe sio mtu wa kawaida"
"waat?"
"ndio hivyo na kama unataka kuniua niue tu,najua unaweza na una nia mbaya na mimi niue sasaa,,najua wewe ni ji.."
kabla hajamalizia sentensi yake Husna alimnasa kibao cha nguvu Roy akaangukia Kitandani.
"unataka kujua ukweli,mimi ni jini sikatai ila ningekuwa nataka ufe nisingekuokoa kwenye ajali boss wako alitaka kukutoa kafara ungeshakufa wewe mimi ndio nimekuokoa"
"unasemaje?"
"wewe hujiulizi watu wote umepona wewe tu kwenye ajali mbaya kama ile?"
Roy alizidi kuchanganyikiwa,kitendo cha husna kutamka kuwa yeye ni jini hakikumshtua sana,kilichokuwa kinamtatiza ni swala la boss wake.
Alimgeukia Husna aliekuwa ameegemea mlango analia akamshika mkono wakakaa kitandani uku anam'bembeleza.
Husna aliponyamaza Roy alimwonyesha meseji aliyotumiwa na bos wake.Husna alicheka akamwambia asihofu kwani hakuna kitakachomkuta.
"sawa ila naogopa utanidhuru"
"siwezi kukudhuru Roy,ata ukiamua kuniacha nitaridhika tu kama hujanipenda sikulazimishi"
"alafu kuhusu ile ajali kuna kitu kila nikitaka kuongea nashindwa"
"kitu gani niambie"
"sintaweza mdomo utakuwa mzito najua"
"leo utaweza"
"Tuliposikia tairi limepasuka kabla gari halijapinduka,Niliona watu wawili wakiwa wamevalia kanzu nyeusi wakiwa na mapanga wanawacharanga abiria yani mpaka gari linapinduka watu wengi walishakatwa katwa na wale watu wawili"
"sasa mbona umeweza?"
"ata mimi nimeshangaa,nilitaka kuwaelezea polisi nikashindwa.
Husna alicheka akamwambia ile ajali ilikusudiwa,na ajali nyingi zinapotokea sio kweli kwamba vioo ndio huwa vinawakata watu bali ni mapepo yanayotaka damu.
"Niliogopa sana"
"wale ni aina ya majini sintakwambia majina yao,hujawahi kuona ajali mtu amekatika mguu,mkono au shingo imeachana na kiwili wili?
"Ndio inatokeaga"
"sasa jiulize kioo gani kinamkata mtu kiasi hicho"
Roy alimsikiliza Husna kwa makini akatikisa kichwa na kukubali kuwa kweli dunia ina mambo.
* * *
Baada ya siku mbili Husna alimwambia Roy kuwa jioni ya siku hiyo anataka kumtoa out ila hakumwambia anapompeleka,Roy alipojaribu kumuuliza Husna alimwambia kuwa ni saprise.
Waliondoka wote pamoja na Mariam wakaelekea mjini kwa ajili ya kufanya Shoping.Waliingia kwenye maduka makubwa ambayo Roy hakutegemea kuwa waafrika wanaingiaga yaye alijua maduka kama yale ni ya wazungu.
Baada ya kila mtu kuridhika na vitu alivyonunuliwa walirudi nyumbani kujiandaa na saprise ambayo Husna aliwaambia anawapeleka usiku wa siku hiyo.
Saa tatu usiku walianza kujiandaa.Mariam alipendeza sana,Roy pia Husna ndio kabisa ama kweli shoping waliokuwa wamefanya mchana haikuwa ya kitoto ila mpaka wakati huo hakuna aliekuwa anafahamu wanapopelekwa.Roy kidogo alianza kuwa na uoga akauliza
"tunaenda na gari?"
"ndio ila tukitoka apo getini nitawafumba macho kwa kitambaa msione ninapowapeleka na nitawafumbua tukifika.Mariam alifunga geti kisha akapanda kwenye gari ambapo husna aliwafumba macho na safari ikaanza lakini Roy hakuwa na amani kabisa moyoni mwake..

Itaendelea

posted from Bloggeroid

0 comments:

Post a Comment