Mabingwa
watetezi wa kombe la FA, Arsenal itapambana na Manchester United katika
hatua hiyo ya nane bora. Arsenal watasafiri kwenda Old Trafford
kuikabili Manachester United katika mchezo wa robo fainali
zitakazochezwa tarehe 7 au 8 ya mwezi Machi.
Manchester United ilijihakikishia nafasi hiyo ya hatua ya nane bora baada ya kuishindilia Preston North End mabao 3-1. Mpambano kati ya Arsenal na Manchester United unatajwa kuwa mkali katika hiyo.
Liverpool
itakuwa mwenyeji wa Blackburn, Bradford City itapambana na Reading
wakati wapinzani wa jadi kutoka West Midlands Aston Villa na West Brom
zitamenyana katika uwanja wa Villa Park.
Hatua ya robo fainali kwa
timu ya Liverpool itampa matumaini nahodha wake Steven Gerrard kucheza
fainali katika uwanja wa Wembley ukiwa ni msimu wake wa mwisho kuwa
katika kikosi cha Liverpool, japokuwa watatakiwa kuishinda Blackburn
ambao tayari waliwatoa nje ya kinyang'anyiro cha kombe la FA Swansea na
Stoke timu za ligi kuu ya England msimu huu.
Timu kutoka daraja la kwanza
Bradford imetinga robo fainali za Kombe la FA ikiwa ni mara ya kwanza
tangu ilipofanya hivyo mwaka 1976, na itakuwa inajiamini kusonga mbele
zaidi baada ya kuzichapa timu za ligi kuu za Chelsea na Sunderland
katika hatua zilizopita.
Ratiba ya michezo ya robo fainali za kombe la FA inaonyesha kuwa:
0 comments:
Post a Comment