Winga Saimon Msuva jana alifunga bao lake la 24 tangu amejiunga na klabu hiyo 2012 akitoke Moro Unied.
Msuva alifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Na kwa ushindi huo wa mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.Yanga SC inapanda kileleni kwa kutimiza pointi 28 baada ya kucheza michi 14,hivyo kuwazidi mabingwa watetezi Azam Fc kwa pointi mbili.
Mabao yote ya Msuva jana yalitokana na kona maridadi za kiungo Mbrazili,Andrey Countinho ambaye pia alisababisha bao la tatu,Countinho alipiga bao ambalo lilimbabatiza beki wa Prisons,Lugano Mwangama na kutinga nyavuni.
Tangu amejiunga na Yanga SC,akisajiliwa kama mchezaji wa timu vijana kutoka Moro United,Msuva amekwisha ichezea timu hiyo mechi 86.
Mabao hayo yalifuta ukame wa mabao wa kinda huyo uliodumu tangu Januari-kwani kwa kipindi chote hicho ameshuudiwa akikosa mabao ya wazi.

0 comments:
Post a Comment