kumekucha msimbazi

Author
Ule msemo wa mwenzio akinyolewa wewe tia maji umezidi kujikita kwenye soka la bongo, na hii ni baada ya kocha wa Simba Sports Club Mzambia Patrick Phiri na benchi lake la ufundi kutimuliwa katika klabu ya Simba.
Phiri ametimuliwa Simba ikiwa Simba ni siku chache tangu kocha wa Yanga Mbrazil Marcio Maximo kutimuliwa, baada ya timu yake Yanga kufungwa na Simba iliyokuwa ikiongozwa na Phiri kwenye mchezo wa nani mtani jembe.
Uamuzi huo umefikiwa jana ikiwa ni matokeo azimio la kikao cha uongozi wa juu wa Simba, na rais wa wekundu wa msimbazi Evans Aveva hii leo anategemea kumalizana rasmi na Phiri, kwa maana ya kutenguwa mkataba.
Nasafi ya Phiri imechukuliwa na kocha Mserbia Goran Kopunovic, kocha huyo amewahi kuifundisha timu ya Police ya nchini Rwanda, na kocha huyo atakapotua rasmi katika klabu ya Simba atasaidiwa na kocha Mrwanda Jean Marie Ntagawabila.

0 comments:

Post a Comment