MARAFIKI CLUB-03

Marafiki CLub~3
By Sparner Boy 0765148781
ilipoishia..
Roy alishtuka sana na kabla hajasema chochote
baba Rehema alimpiga teke la kwenye mbavu
iliyomfanya aanguke chini kama mzigo na hapo
hapo mama Rehema akatokea uku anapiga
makofi..
Endelea..
Roy akiwa pale chini uku suruali yake bado
ikiwa chini ya magoti,baba Rehema alianza
kumshushia kipigo mda huo Rehema alikuwa
pembeni akilia.Ni kweli mchezo ule walipanga
ili kumkamata Roy ila kwa kipigo alichokuwa
anakipata roho ya huruma ilimwingia Rehema
na kujikuta anashindwa kuzuia machozi.
Baada ya Roy kuwa hoi kwa kipigo baba
Rehema aliwapigia simu polisi wakaja
kumchukua tayari kumpeleka Kituoni na
aliwaambia polisi
"naomba msimuachie huyo kanibakia binti
yangu na kumjaza mimba"
"hatatoka huyu miaka 30 inamuhusu"
Alijibu polisi mmoja aliyeonekena kuwa na
kihere here kuliko wenzake.
Roy alibebwa mseke mseke akatupwa kwenye
gari la polisi akiwa hajiwezi.Wakiwa njiani polisi
mmoja akasema
"huyu kijana amepigwa sana afande asije
akatufia"
"anajidai huyu hajapigwa,oyaa..wakati
unaingiza tamu ee,maisha yako yaliyobaki apa
duniani unaenda kumalizia jela"
Polisi waliendelea kumsuta Roy bila huruma na
ndani ya muda mfupi walifika kwenye kituo cha
polisi.Walimwamuru ashuke ambapo Roy
alijitahidi kuinuka pale chini bila
mafanikio,polisi mmoja alipandwa na hasira
kwa kitendo kile aliona Roy anawapotezea
muda.Alimpiga teke la kwenye mbavu pale pale
alipopigwa na baba Rehema ambapo Roy
alipiga ukelele mara moja na kunyamaza
kimya,wote walishangaa sana kwa kitendo kile
na baada ya kuchunguza waligundua kuwa
kijana yule alikuwa amepoteza fahamu na bila
kupoteza muda wakaelekea hospital kwa ajili ya
kuokoa maisha yake.
Mama Roy alichanganyikiwa baada ya kusikia
kilichomkuta mwanae.Aliilaani familia ya
Rehema kwa kitendo alichokiita ni uonevu kwa
sababu yeye alikuwa ni mjane na usiku huohuo
akawahi hospital.Alipofika alimkuta Roy bado
hajapata fahamu alikuwa bado ametundikiwa
dripu,mama yule hakuamini aliangua kilio uku
analalamika sana.Madaktari walikuja na
kumtuliza uku wanamtia moyo kuwa Roy
atapona.Mama yule alipoacha kulia daktari
alimuita ofisini
"mama pole kwa yaliyokukuta,umesema huyu
ni mtoto wako wa pekee"
"ndio yani hawa watu..."
"baasi nyamaza,kijana wako kampa binti
mwenye umri chini ya miaka 18
mimba,kisheria inahesabika amebaka hivyo
miaka 30 jela itamuhusu ila nataka nikusaidie"
"nisaidie daktari mwanangu asiende jela
jamani"
Daktari kwa kumuonea mama Roy huruma
alimsaidia ambapo Roy alipopata fahamu
majira ya saa nane za usiku,walimtorosha na
kumpeleka nyumbani kwa daktari yule kwa ajili
ya kuendelea na matibabu na polisi walipokuja
asubuhi madaktari walisema kuwa Roy
alitoroka bila wao kujua na haikujulikana
alipoelekea .
"mmefanya uzembe muhalifu akatoroka"
"samahami afisaa,kazi yetu ni kutibu wagonjwa
na sio kulinda kwa hiyo tunaomba mkamtafute
mtu wenu acheni fujo hapa ni hospital"
* * *
Zilipita wiki mbili Roy akiwa nyumbani kwa
daktari akipata matibabu na hali yake kwa
ujumla ilianza kutengemaa.Kwa kuwa polisi
bado walikuwa wanamtafuta mama Roy na
daktari walimkalisha Roy chini na baada ya
kumuelezea kila kitu kinachoendelea Roy
alisema anataka kwenda Tanzania kwa shangazi
yake kujificha kwani uko ni vigumu polisi
kumkamata.
Mama Roy na Daktari walikubaliana na wazo
lile na baada ya wiki moja Roy alielekea kwa
Shangazi yake aliekuwa anaishi usariver
Arusha.
Roy alifurahi sana kufika Tanzania,ilikuwa mara
yake ya pili,kwa mara ya kwanza alikwenda ila
alikuwa mdogo sana.
Joan na marafiki wengi wa Roy wanaoishi
Tanzania walifurahi sana baada ya kusikia rafiki
yao amekwenda Nchini kwao.
Baada ya miezi sita kupita Roy alishapazoea ana
kuanza kuwa mwenyeji,alikuwa anafanya kazi
ya kukaanga chips katika bar moja kazi
aliyokuwa ametafutiwa na shangazi
yake.Hakuwa mtu wa kukaa nyumbani tena
sasa akawa ameanza kujitegemea peke yake.
Siku moja alichelewa sana kutoka kazini
kutokana na wingi wa wateja,Alipofunga kazi
majira ya saa tano kasoro usiku,alijiandaa
akaelekea stand ambapo haikuwa mbali sana na
anapofanyia kazi.Alipofika Stand hakukuta mtu
yoyote,wakati bado anasubiri gari alikuja dada
mmoja na kufanya idadi wao kuwa wawili,kwa
haraka haraka binti yule alionekana ni mtu
aliekuwa ameshikilia sana Dini ya kiislam
kutokana na mavazi yake.Walisimama pale
stand kwa muda mrefu bila gari yoyote
kutokea,Roy alipomwangalia dada yule vizuri
aligundua kuwa alikuwa mrembo kupita kiasi
ila alishindwa kuelewa kuwa usiku ule mrembo
yule alikuwa ametoka wapi.wakati mawazo yale
yale bado yanaitawala kichwa chake alisikia
sauti nzuri na ya upole iliyopenya kwenye
masikio yake
"kaka tutapata gari kweli"
"sidhani ila ngoja tusubiri"
"jamani ntaenda wapi mimi"
Roy alimuangalia dada yule akajikuta akisisimka
gafla kwani alikuwa mzuri ajabu na pale pale
akili yake ikaanza kufanya kazi namna ya
kumpata,alishangaa kwa nini wazo lile lilimjia
haraka kiasi kile na moyoni akawa anaomba
gari lisitokee,,,
Itaendelea

posted from Bloggeroid

No comments:

Post a Comment