Marafiki Club~8
By Sparner Boy 0765148781
Ilipoishia
Baada ya Mariam kufunga geti alipanda kwenye gari,kabla Husna hajaondoa gari aliwafumba macho na kuondoa gari taratibu huku Roy akikosa amani moyoni mwake..
Endelea..
Ilipita nusu saa wakiwa wanasafirii,Roy alichoka kutembea huku haoni na alipotaka kutoa kile kitambaa ili aweze kuona,Husna alikuja juu sana akamwambia
"Huby kama unataka ubaya na mimi fanya hivyo uone"
"kwa nini Hatufiki?"
"tumefika ni hapo mbele pia naomba uwe mtulivu kama mwenzako Mariamu"
Roy alikaa kimya,muda mfupi baadae gari lilianza kupunguza mwendo na kusimama haraka Husna alishuka kisha akawashusha wote na kuwafumbua macho yao ambapo walijikuta wapo nje ya jengo moja kubwa na nzuri sana,waligundua kuwa ni club ya usiku kutokana na maandishi yaliyokuwa yameandikwa mlangoni "Marafiki Club".
Mariam alifurahi sana akawa anamshukuru Husna kwa kuwapeleka sehemu kama ile,Kwa upande wa Roy alibaki kimya anaangalia jengo lile ambapo watu walikuwa wanaingia na kutoka wakiwa busy na kuonekana kutowajali wao kwani walikuwa wanamsalimia Husna tu.
Wakati bado anashangaa jengo lile Husna alimshika mkono wakaingia ndani huku Mariam ana wafuata kwa nyuma.
Huko ndani watu walikuwa wengi wanacheza mziki na wao wakajumuika nao ila Roy wakati anaangaza macho mle ndani na namna watu wanavyocheza aligundua pale sio sehemu ya kawaida pia watu waliomo mle ndani sio wa kawaida,Alianza kutetemeka kwa uoga akamwangalia Mariamu aliyekuwa pembeni anacheza peke yake bila wasiwasi wowote.Wakati wanaendelea kucheza mziki alikuja baba mmoja wa makamo akamuomba Husna watoke pembeni kwani alikuwa na maongezi nae.Husna limgeukia Roy akamwambia
"Huby naomba nizungumze nae usihofu narudi sasa hivi"
"sawa utanikuta nakusubiri"
Alijibu Roy kwa unyonge.
Husna alipoondoka na baba yule,Roy alimtoa Mariam pembeni akamwambia
"apa ni wapi Mariamu naona huna wasiwasi ata kidogo"
"sielewi kaka Roy yaani pazuri ila watu hawaeleweki"
"hii club sio ya kawaida niamini mimi,angalia tulivyoingia kimahajabu ajabu kuwa makini"
"sawa kaka Roy nimekuelewa"
Wakati Roy na Mariamu wanaongea,Husna alirejea ila hakuwa na raha kama mwanzo alivyoondoka na yule baba kibaya zaidi alikuwa na alama ya vidole usoni kitendo kilichoanishiria kuwa amepigwa makofi ya uso, kutokana na uweupe wake hakuna kitu kilichokuwa kimejificha.Roy alimvuta pembeni akamuuliza
"nani amekupiga hivi"
"twendeni nyumbani"
"utapigwaje ukiwa na mimi Husna niambie nani amekupiga twende ukanionyeshe"
"Roy hutaweza watakuuwa,uku wewe najua hupafahamu ila siku moja utaujuwa ukweli cha kufanya twendeni nyumbani mi nipo salama"
"hapana Husna nataka kujua nani kakupiga,nisubirini hapo"
Alizungumza Roy kwa hasira akaondoka na kuwaacha Husna na Mariam wakimsubiri.
Alienda counter akamkuta dada mmoja wa kiarabu,baada ya kusalimiana yule dada akamuuliza
"unataka kinywaji gani kaka"
"nipe pombe yoyote kali nataka nilewe kwa haraka sana"
"pombe,we umetoka wapi unaulizia pombe humu ndani au umechoka na maisha?"
"dada nipe pombe hii ni disco,kuna disco isiyouza pombe we chizi nini"
"mi nani"
Kabla Roy hajajibu Husna alifika akakuta mabishano yale,Yule dada alikuwa amekasirika ila Husna akawa anamuomba asimwambie mkuu
"mkuu wa wapi,namtaka huyo mkuu kwanza apa ni wapi umenileta Husna unanipeleka peleka sijielewi?"
Roy aliendelea kuongea kwa hasira sana uku anatukana matusi na watu wakawa wanazidi kujikusanya kumuangalia Roy aliekuwa kama amechanganyikiwa.Husna alipooma Roy anazidi kuwa na jazba kadri muda ulivyokuwa unaenda,alimfuata akamgusa kichwani pale pale Roy akaanguka chini na kupoteza fahamu.
Watu walikuja juu wakitaka kumuuwa Roy kwa kitendo cha kuulizia pombe na kumtusi mhudumu wao ila Husna akajitahidi kuwaomba wasifanye hivyo.Mwisho walimuelewa kwa shingo upande wakam'beba Roy na kumpakiza kwenye gari.Kabla safari haijaanza Husna akamwambia Mariam
"unatakiwa kufumba macho sitaki upafahamu apa kwa sasa ivi sawa?
"mmh dada jamani kwa nini?"
"fuata ninachokuambia Mariam"
Husna aliongea kwa Hasira mpaka Mariam akaingiwa na hofu kwani hakuwahi kumwona boss wake akiwa katika hali ile.Alichukua kile kitambaa akakifunga kujiziba macho na safari ya kurudi nyumbani ikaanza.
Walipofika walisaidiana kum'beba Roy na kumuingiza ndani kisha Mariam akaelekea chumbani kwake kwa ajili ya kujipumzisha.
Roy alishtuka asubuh majira ya saa mbili Husna akiwa amemlalia kifuani,wakati bado anajiuliza amefika vipi nyumbani wakati alikuwa disco,Husna alimwuliza
"unajiskiaje?"
"poa tu"
"Roy tumefanya kosa kubwa sana ambalo litatugharimu maisha yetu"
"kosa gani,maisha yetu?"
"ndio,siunakumbuka jana nilivyoondoka na yule baba nikarudi nikiwa na alama ya vidole kwenye mashavu yangu,alinipiga sana"
"kumbe ni yule mzee ndio alikupiga,nipeleke kule nikamfundishe adabu"
"Roy nyamaza ivi unajua yule ni nani?"
"hapana kwani ni nani?"
Aliuliza Roy kwa shauku kubwa uku anasubiri Husna amjibu na mda huo Roy hasira zilianza kumpanda..
Itaendelea..

posted from Bloggeroid
No comments:
Post a Comment