JKT Ruvu yaikamia Kagera Sugar

Author

BAADA ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbeya City, timu ya JKT Ruvu imesema imejipanga zaidi kwa mchezo wake ujao dhidi ya Kagera Sugar.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Mkuu wa maafande hao Fred Minziro alisema katika mechi zao mbili zilizopita matokeo hayakuwa mazuri, hivyo wanategemea kikosi chake kitafanya vizuri katika mchezo huo.

Alisema kuna baadhi ya mapungufu ambayo anakusudia kuyarekebisha katika kukiweka sawa kwa lengo la kuleta ushindi.

“Tumefanya vibaya michezo iliyopita, tunahitaji kubadilika kama tunataka kuwa katika nafasi tatu za juu, nategemea katika mchezo ujao mambo yatakuwa mazuri,”alisema.

Alisema Kagera Sugar sio timu rahisi, ina ugumu wake kwani katika mchezo wa raundi ya kwanza waliwafunga mabao 2-0. Minziro alisema awamu hii watalipiza kisasi, hawatakubali kufungwa mabao tena na timu hiyo katika mchezo huo wa pili.

JKT Ruvu kwa sasa ina pointi 19 kwenye msimamo wa ligi na imekuwa ikikimbizana na Mtibwa Sugar katika pointi.

0 comments:

Post a Comment