
Bunge la Ujerumani linatarajiwa kupigia kura mpango wa kurefusha muda wa kutoa msaada wa fedha kwa Ugiriki kwa kipindi cha miezi minne mingine.
baadhi ya Wabunge wa Ujerumani wameshuku kuhusu mpango huo ambao unaelezwa kuwa utaweza kupita kirahisi.
Hatua hii inakuja baada ya Polisi na Waandamanaji kupambana wakati wa Maandamano mjini Athens siku ya Alhamisi.
Hizi ni vurumai za kwanza tangu Chama cha Mrengo wa kushoto cha Ugiriki Syriza kuongoza Serikali kuu ya Ugiriki.
Wanaharakati waliwarushia mabomu ya Petroli na mawe Polisi na kuchoma moto magari baada ya Matembezi yaliyohusisha mamia ya Waandamanaji.
Mpango wa kupata mkopo pia umetikisa Chama cha Syriza.
0 comments:
Post a Comment